logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Gloria Ntazola asimulia hali halisi baada ya mzozo na afisa wa kanjo

kulingana na yeye,afisa huyo wa kanjo aliingia ndani ya gari lake kwa laziam akitaka kumkamata

image
na Davis Ojiambo

Vipindi23 October 2023 - 11:01

Muhtasari


  • • Katika mahojiano ya moja kwa moja na Radio Jambo,Ntazola amesema alifikia uamuzi huo baada ya maafisa hao kumvamia kwa kuegeza gari lake,baada maafisa hao kuvamia wachuzi wengine.
  • • "Nilimkataza asiingie kwa gari langu lakini akaingia kwa lazima,nilishikwa na hasira na hivyo nikataka kumpa funzo,kwa sababu hii si mara ya kwanza yeye kunifanyia hivyo,"
Gloria Ntazola

Muundaji maudhui na mwanabiashara Ntazola Gloria amesimulia hali halisi aliyokumbana nayo wakati mzozo kati yake na afisa wa kanjo ulitokea hapo awali.

Katika mahojiano ya moja kwa moja na Radio Jambo,Ntazola amesema alifikia uamuzi huo baada ya maafisa hao kumvamia kwa kuegeza gari lake,baada maafisa hao kuvamia wachuzi wengine.

Gloria,amesema wazi kuwa afisa huyo alikuwa na mazoea kwani hii haikuwa mara yake ya kwanza kumfanyia tendo hilo la kuitisha hongo kila wakati akiegeza gari lake.

Kulingana na yeye,afisa huyo wa kanjo aliingia ndani ya gari lake kwa laziam akitaka kumkamata kwa sababu ya kuegeza gari bila kulipia akajaribu kumkanya ila akasisitiza.

"Nilimkataza asiingie kwa gari langu lakini akaingia kwa lazima,nilishikwa na hasira na hivyo nikataka kumpa funzo,kwa sababu hii si mara ya kwanza yeye kunifanyia hivyo,"alisema.

Mwanabiashara huyo anayeendesha biashara ya vipodozi,amesimulia jinsi maafisa hawa wa kanjo wanaghadhabisha watu wakati wanapofanya shughuli za ushuru jijini.

Vilele amedhibitisha kuwa hasira yake ilijumuishwa pamoja na taarifa ya hapo awali mbapo maafisa hao walikuwa wamewadhulumu wachuuzi katika jiji na hivyo kupelekea kumuadhibu afisa huyo kwa kumpeleka safari ambayao hakuwa ametarajia.

Ntazola anasema alipokea simu kutoka kwa polisi ya kumtaka kuandikisha tarifa,na kusema kuwa kwa sasa polisi wanaendesha uchunguzi ili kubaini  yupi aliyekuwa na makos.

Aidha ameoma msamaha wake kwa wakenya na mashabiki wake kwa jumla kwa matusi aliyotamka akiwa hewani akisema kuwa yalichangiwa na kupandwa mori.

Ntazola sasa amesema yuko tayari kuwa na mazungumzo na afisa huyo ili kuomba msamaha ikiwa atapatikana na makosa baada ya uchunguzi kumalizika.

 

 


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved