logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: "Alinikata kidole haisimamangi" Wanandoa wahusika vita vya visu baada ya kuzozana

Anthony alisema siku ambayo walikosana Rose alifika nyumbani akiwa mlevi na kuanzisha vita.

image
na Samuel Maina

Vipindi03 May 2023 - 06:19

Muhtasari


  • •Rose alisema alizozana na mzazi huyo mwenzake Oktoba mwaka jana baada ya kuchelewa kuingia kwa nyumba.
  • •Anthony alipopigiwa simu, mwanadada huyo alichukua fursa kumuomba radhi ila akakana kutenda kosa lolote.
Gidi na Ghost

Kwenye kitengo cha Patanisho, mwanadada aliyejitambulisha kama Rose Kamathi ,23, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mumewe Anthony Murimi ,24, ambaye alikosana naye mwaka jana kufuatia ugomvi wa kinyumbani.

Rose alisema alizozana na mzazi huyo mwenzake Oktoba mwaka jana baada ya kuchelewa kuingia kwa nyumba.

"Nakumbuka ilikuwa siku ya Jumapili. Saa moja jioni ndio tulimaliza mkutano wa chama. Tulikuwa tunasambaza mchele. Siku hiyo nilikula nikapeleka mchele nyumbani. Sikuwa nimepika nikaenda kununua kitu ya kupika. Nilirudi kwa nyumba kitu saa mbili unusu. Akaniuliza nimetoka wapi nikamwambia nimetoka soko. Hapo ndio tulianza kuzozana hadi tukapigana hadi nikaenda kwa chifu. Akaambiwa kama hanitaki anipatie nguo niende na akanipatia. Bado nampenda na hata mtoto anashinda akimtaja," Rose alisema.

Rose aliweka wazi kwamba angali anampenda Bw Anthony licha ya ndoa yao kugongwa mwamba mwaka jana.

"Hatujawahi kuongea na yeye lakini kuna wakati mtoto alikuwa mgonjwa, nikimpigia simu anakataa kushika. Kuna wakati nilimpigia nikamwambia mtoto ni mgonjwa akaniambia nishughulike mwenyewe," alisema.

Anthony alipopigiwa simu, mwanadada huyo alichukua fursa kumuomba radhi ila akakana kutenda kosa lolote.

"Nilikuwa nataka kuomba msamaha lakini Mungu anajua ukweli hakuna chenye kilifanyika kama unavyofikiria. Huyu mtoto anakuhitaji na anataka tumlee tukiwa wawili," Rose alimwambia mzazi huyo mwenzake.

Anthony hata hivyo aliweka wazi kwamba tayari amefanya maamuzi ya kuishi maisha yake bila Rose.

"Mimi niliona ikuwe hivyo. Nilishaamua na nikasonga mbele na maisha yangu. Nikuulize, tangu uende umewahi kunipigia ukaomba msamaha?," alisema.

Alidai kuwa siku ambayo walikosana Rose alifika nyumbani akiwa mlevi na kuanzisha vita iliyopelekea wao kukosana.

"Alikuwa amelewa alafu akaniletea vita hadi akanichukulia kisu na kunidunga. Alienda kwa polisi akasema mimi ndio nilianzisha vita nikamdunga na kisu.Ilifika mahali nikaambiwa na mzazi niachane na yeye ni kisirani. Ilifika mahali nikaona tu niachane na yeye. Wakati atakubali kusema ukweli akuje kwa wazazi aombe msamahe aseme. Mimi sina shida na mtoto ," Anthony alisema.

Rose alijitete kwa kusema, "Hakuna kitu ambayo iliendelea hapo. Lakini wewe ulisikiliza maneno ya watu wakatutenganisha.  Hiyo kisu nilikuwa nataka kukata kitunguu nayo. Sasa nakuchukulia kisu na nimezaa na wewe." 

Aliongeza, "Amenikata kidole hadi nimeshonwa. Hata kidole moja haisimamangi. Anavyosema nilimkata ni uongo. Tulikuwa tunang'ang'ana kama nimeshika kisu. Alikuja akanishika kama napika ugali."

Rose pia alikana madai ya kuwa mlevi huku akibainisha kwamba hajawahi kunywa pombe ila gauarana mbili.

Pia alikataa agizo la Anthony la kutembelea wazazi wake ili kuomba msamaha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved