Katika kitengo cha patanisho bwana Victor alituma ujumbe apatanishwe na mkewe Carol ambaye walikosna na kumuachia watoto.
"Nilikosana na mke wangu, na akaenda kwko nilipopigia wakwe wangu waliniambia kwamba hawajui mahali alipo bali walimtafutia kazi nairobi
Aliniacha na watoto, nikimpigia simu anasema kila wakati atarudi lakini harudi,pia niliona jumbe akiwa amemwambia mwanamume kwamba wanaweza patana nairobi kwa maana amepaa kazi huko
Mimi sijui ni kosa gani ambalo nilifanya ili aondokee kwangu," Alieleza Victor.
Baada ya kufanya juhudi zetu za kumpigia mkewe simu alikuwa na haya ya kusema.
"Mwanamume huyo alinichapa baada ya kwenda kanisani karibu meno yatoke kutokana na kichapo ambacho alinipa
Alikuwa anasema kuwa ni yeye atanipa ruhusa ya kuenda kanisani,na pia kwamba nikienda kanisani narudi na vitina
Kurudi nitarudi Aprili 9,"