Patanisho:Nilimfumania mke wangu na mwanamume mwingine kitandani

Muhtasari
  • Nilimfumania mke wangu na mwanamume mwingine kitandani
Ghost na Gidi
Image: Studio

Katika kitengo cha patanisho bwana Michael alituma ujumbe ili apatanishwe na mkewe ambaye alimvumania na mpango wake wa kando alipokuwa anatoka kazi.

Kulingana na bwana huyo hakuleta vurugu yoyote ilhali aliwaacha waendelee na kitendo chao.

"Naomba mnipatanishe na mke wangu wa miaka 10. Nilikuwa ninafanya kazi nje na kuja nyumbani baada ya miezi 2.

Siku moja nikarudi bila kumwambia nikampata na mwanaume mwingine kitandani... Sikuleta vurugu, nikamwambia wakimaliza waende mimi nikaondoka, akabeba vitu akaondoka

Aliniwachia watoto wawili baada yake kuondoka, ndio nilikuwa nalewa lakini niliacha nimeokoka sasa

Nilioa mke wa pili ambaye aliaga dunia baada ya kusumbuliwa na ujauzito," Alieleza.

Baada ya kufanya juhudi za kumfikia mke wake alikuwa na haya ya kusema;

"Huyu mwnamume alikuwa na mpango wa kando, ameuza shamb yote, pia alioa mwanamke mwingine na akaaga dunia huyo ni Mungu alikuwa amekataa, sitaki kurudiana naye,"

Kwa mengi zaidi tembelea radiojambo youtube.