'Mpango wa kando aliniambia najilazimisha kwa bwanangu, eti nazaa kama panya' Mwanamke asimulia masaibu yaliyokumba ndoa yake ya miaka 8

Muhtasari

•Atieno alisema kwamba walikosana na mumewe baada yake kugundua kwamba ndoa yake ya miaka nane imekabiliwa na misukosuko si haba kwani mumewe amekuwa akicheza karata nje.

•Atieno alisema kwamba mwanamke yule ambaye alishuku kuwa mpango wa kando wa bwanake aliwahi kumtumia ujumbe wa matusi  kwa simu kuhusiana na uhusiano wake na mumewe.

•Bwana Otieno alipopigiwa simu alipuuzilia mbali madai ya mkewe kuwa ana nia ya kuoa mke wa pili  na kudai kwamba hana mpenzi mwingine.

Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha Gidi na Ghost asubuhi kitengo cha Patanisho mwanadada aliyejitambulisha kama Coleta atieno 28, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mumewe Charles Okoth 38 ambaye wamekuwa kwa ndoa kwa miaka 8 na kubarikiwa na watoto wanne pamoja.

Akoth alisema kwamba walikosana na mumewe baada yake kugundua kwamba ndoa yake ya miaka nane imekabiliwa na misukosuko si haba kwani mumewe amekuwa akicheza karata nje. 

"Tumekuwa na shida tangu tupatane na huyu mzee. Alinioa nikiwa kidato cha tatu. Nilikuwa naishi pekee yangu kwani tangu babangu aage hakuna ambaye angeweza kunilipia karo, nilikuwa nafanya kazi ya kijakazi kisha naenda shule. Tulipopatana na yeye tulikubaliana atanioa na angemalizia kunilipia karo.

Tumekaa miaka nane kwa ndoa lakini kwa hakika hiyo miaka yote hakuna wakati nimekaa na amani, yeye ni mtu ako na macho ya nje Nimejaribu kuongea na yeye  na hata ndugu zake lakini hajabadilika" Atieno alisimulia.

Mwanadada huyo alisema kwamba hivi karibuni alichukua simu ya mumewe na kupata ujumbe ambao alishuku ulikuwa umetoka kwa mpango wake wa kando. Alidai kwamba wamewahi kuzozana tena na mumewe kwa sababu ya mwanadada ambaye alikuwa amemtumia ujumbe.

"Nimepata kuwa bado anaendelea na mwadada yule yule. Nilikuwa nataka nijue ako na mawazo gani. Kama ameamua kuwa na bibi mwingine mimi  siko tayari aniachie nafasi kwa upande wangu mimi nikae na watoto wangu" Atieno aliambia Gidi.

Atieno alisema kwamba mwanamke yule ambaye alishuku kuwa mpango wa kando wa bwanake aliwahi kumtumia ujumbe wa matusi  kwa simu kuhusiana na uhusiano wake na mumewe.

"Huyo mwanamke alinitusi kwa simu akaniambia eti mimi ni mke wa aina gani nilijilazimisha kwa bwana mwenye ata hajui njia ya kuenda kwetu, eti nazaazaa kamapanya. Hiyo inamaaanisha kuwa huyo bwana ndiye alienda kwake akamwambia kwamba hajawahi kuenda kwetu na nazaazaa kama panya" Alisema Atieno.

Mwanamke huyo alisema kwamba baada ya mumewe kugundua kuwa huwa anafuatilia mazungumzo yaliyo kwenye simu yake aliweka namba ya siri kila mahali ili asiweze kumchunguza tena.

"Ameweka namba ya siri ila mahali. Mimi simu yangu iko wazi  huwa inashinda hapo. Kwa nini yeye aniwekee namba ya siri kila mahali.. Juzi nilimwambia kwamba nampenda sana lakini shida yake ni kutokuwa mwaminifu alafu akaniambia eti mwanaume lazima awe na wazo la pili.. Ananiumiza roho kila siku, huyo mtu amefanya nimepigana na wasichana huku mtaani hata nimechoka" Atieno alisimulia.

Bwana Otieno alipopigiwa simu alipuuzilia mbali madai ya mkewe kuwa ana nia ya kuoa mke wa pili  na kudai kwamba hana mpenzi mwingine.

"Kama huyo  mmoja ni ngumu kumlisha, sasa huyo mwingine vipi. Ile mali niko nayo ni ya huyu mwenye amenileta Radio Jambo" Otieno aliambia Gidi.

Otieno alisema kwamba alifunga simu yake na nambari za siri kwa kuwa mkewe alikuwa akimchunguza sana.

'"Hiyo ndiyo shida yake kutoka kitambo kuchokora simu yangu akitaka kujua kila namba ni ya nani. Akipata ujumbe anasema nimepatikana" Otieno alisema.

Hata hivyo alikubali kutoa nambari za siri ambazo alikuwa ameweka ili kupatia mkewe utulivu wa moyo.