Patanisho: "Aliyekuwa mke wa bwanangu aliniambia anarudi nimsongee" Mwanadada azungumzia wasiwasi kuhusu ndoa yake

Muhtasari

•Caroline alikuwa na wasiwasi kuhusu ndoa yake kwani alihofia kwamba aliyekuwa mke wake kwanza wa mumewe Antony Omondi alikuwa na nia ya kurejea tena.

•Caroline alisema kwamba waliwasiliana na mwanamke yule na akamuarifu amsubiri kwani alikuwa na mpango wa kurejea.

•Anthony alisema kwamba hakuna uwezakano wake kumrejesha yule mwanamke kwani aliondoka miaka minne iliyopita na hajui alikokuwa.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha 'Gidi na Ghost asubuhi' kitengo cha Patanisho mwanamke aliyejitambulisha kama Caroline alituma ujumbe akiomba kupata hakikisho kutoka kwa mumewe.

Caroline alikuwa na wasiwasi kuhusu ndoa yake kwani alihofia kwamba aliyekuwa mke wake kwanza wa mumewe Antony Omondi alikuwa na nia ya kurejea tena. Alidai kwamba ugomvi kati yao ulianza mwezi mmoja uliopita na hakukuwa na amani kwa ile boma,

"Ningependa kujua msimamo wake maanake nilipopatana naye kuna mwanamke alikuwa ameoa hapo awali. Walikuwa wamepata naye mtoto mmoja. Wakaachana alafu akaenda akakaa nje kama miaka tano hivi. Antony akaniambia atanioa kabisa kwa sababu yule bibi wa kwanza alikuwa ashaolewa kwingine. Lakini huyo bibi alimpigia simu eti anataka kurudi tena na alikuwa ameolewa kwingine" Caroline alisema.

Caroline alisema kwamba waliwasiliana na mwanamke yule na akamuarifu amsubiri kwani alikuwa na mpango wa kurejea.

Alisema kwamba tayari walikuwa wamepanga kuenda na Antony nyumbani kwao kuona wazazi mwaka ujao ila sasa ana wasiwasi kuwa huenda hali ikabadilika kama kweli yule mke wa kwanza angerejea.

"Nilipomuuliza Antony aliniambia eti ananipenda mimi lakini siwaelewi. Sikutoka bado kwani nilitaka anioe. Ninampenda kweli sio chocha. Nataka nijue uamuzi wake" Caroline alisema.

Antony alipopigiwa simu alisisitiza kwamba hakuwa na nia ya kumrejesha mke wake wa kwanza ila yeye ndiye alitaka kurudi. 

Anthony alisema kwamba hakuna uwezakano wake kumrejesha yule mwanamke kwani aliondoka miaka minne iliyopita na hajui alikokuwa.

"Yule ndiye anataka kurudi. Alienda takriban miaka minne iliyoenda. Amekuwa wapi? Ako na mtotowangu mmoja huwa tunawasiliana mara moja moja kwa sababu ya mtoto" Antony alisema.

Alisema kwamba walishiriki mazungumzo pamoja na mkewe na aliyekuwa mke wa kwanza ili kutafuta suluhu.

 Antony alisema kwamba anampenda mkewe sana na hata huwa anampatia mshahara yake yote ili apangie matumizi

Caroline aliridhishwa na hakikisho ambalo alipatiwa na mumewe na kudai kwamba anampenda sana Antony.

Alisema kwamba hana tatizo lolote iwapo wawili hao watakuwa wanawasaliana kuhusu mtoto wao wala sio mambo mengine.

"Mimi sina shida waongee. Hata nilimwambia asiweke mtoto hivo amsaidie lakini sio mambo mengine. Huyo mwanamke akiongea anaongea ni kama anakuja. Aliniambia eti anakuja nimsongee. Nimsongee wapi jamani? " Alisema Caroline.

Maafikiano mema yalipatikana kati ya wawili hao na wakahakikishiana kwamba wanapendana sana.