Patanisho:"Amenoa panga akaweka chini ya godoro!" Mama mkwe afichua maovu ya jamaa dhidi ya binti yake

Muhtasari

•Joseph alisema ndoa yao ya miaka minne ilisambaratika miezi miwili iliyopita baada yake kupata jumbe za mwanamume mwingine kwa simu ya mkewe.

•Mama ya Beatrice alifichua kwamba Joseph alikuwa na mazoea ya kumpiga binti yake na alimshtumu kwa kuendeleza ukahaba.

•Mama Beatrice pia alifichua kwamba wakati Joseph alikuwa anaishi pamoja na bintiye alikuwa  ameficha panga chini ya godoro na kutishia kumkatakata mkewe.

Image: RADIO JAMBO

Katika kipindi chetu cha 'Gidi na Ghost asubuhi' kitengo cha Patanisho jamaa aliyejitambulisha kama Joseph Halamisi (29) kutoka Busia alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Beatrice Omutere (24).

Joseph alisema ndoa yao ya miaka minne ilisambaratika miezi miwili iliyopita baada yake kupata jumbe za mwanamume mwingine kwa simu ya mkewe.

Alisema alianza kumshuku Beatrice aliporejea nyumbani kutoka mahali alikuwa ameenda kazi kwani hakuwa anampa nafasi ya kushika simu yake.

"Ilikuwa mwezi Novemba. Alikuwa anaenda kazi pande za Komarock. Ni kama vile alikuwa  huko alipatana jamaa mwingine ikawa kwa sishiki simu yake. Akienda kwa choo alikuwa anaenda nayo, akilala anaificha. Nikamuuliza mbona ikawa vile na awali haikutokea. Akaniambia nishughulike na simu yangu nikamwambia ni sawa.

Kuna siku alisahau simu kwa meza.  Nakachukua simu yake ambayo ilikuwa na memory card ili nisikize ngoma. Nilipobonyeza upande wa ngoma nilipata nambari za simu huko nikashindwa hizo ni ngoma za aina gani. Nilipobonyeza nilisikia sauti ya mwanamume. Walikuwa wanaongelea vile wangekuta, walikuwa wanasema eti wakutane ile njia huwa wanakutana na wakuje mpaka kwa nyumba" Joseph alisimulia.

Joseph alisema baada ya kusikiliza mazungumzo kati ya mkewe na jamaa huyo walizozana kisha Beatrice akatoka na kuenda kwao.

Alisema juhudi zote alizokuwa amefanya za kupatana na mkewe ziligonga mwamba kwani Beatrice alikuwa amekataa kabisa kurejea.

"Tulikuwa tunazungumza vizuri na mamake lakini kwa saa hii ata yeye anasema nitafute mke mwingine nioe. Mwanadada naye anasema iko tu vile mama amesema" Joseph alisema.

Juhudi za Gidi kuwapatainsha wanandoa hao zilikabiliwa na changamoto kwani simu ya Beatrice ilikuwa na kasoro.

Hata hivyo Gidi aliweza kumpata mamake Beatrice ambaye alifichua mengi zaidi kuhusu mzozo kati ya bintiye na Joseph.

Mama ya Beatrice alifichua kwamba Joseph alikuwa na mazoea ya kumpiga binti yake na alimshtumu kwa kuendeleza ukahaba.

"Msichana wangu alikuwa anaishi na huyo kijana vizuri. Shida ilitokea wakati huyo kijana alianza kupiga msichana wangu karibu amuue. Mara ya kwanza tulimuachia, mara ya pili tukaambia msichana akuje nyumbani ili kijana aje pia tujue nani mbaya. Ilikuwa kijana aje tuongee. Ata jana alinipigia simu akaniambia anapanga kuja. Nilimwambia akitaka kuja aniambie siku mbili kabla ndivyo nijipange. Alisema angeniambia. Baadae alipigia msichana simu akamwambia aniambie hatakuja. Nilishangaa mbona akasema hivo na tulikuwa tumeongea vizuri tukaelewana. Baadae alinitumia message akaniambia hatakuja. Nilikasirika nikamwambie kama ni hivo akae sitaki mambo yake" Mama Beatrice alisema.

Mama Beatrice pia alifichua kwamba wakati Joseph alikuwa anaishi na bintiye alikuwa  ameficha panga chini ya godoro na kutishia kumkatakata mkewe.

"Alinunua panga akanoa akaweka chini ya godoro. Huwa anasema kuna wakati atakatakata Betty amuweke kwa gunia na aende amtupe kwa bolea. Huwa anaambia mtoto wangu. Amenoa panga akaweka chini ya godoro, huwa anamwabia hiyo panga ni yake" Alisema.

Mama Beatrice alimshauri Joseph ajipange aende nyumbani wazungumze ili warejeshe mahusiano yao