logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho:Nakupenda kama sukuma. Tuma fare saa hii nikuje, ata siogi!- Mwanadada amwambia mumewe

Mwanadada huyo alimwomba mumewe atume nauli na kumhakikishia kuwa angerudi mara moja.

image
na Radio Jambo

Habari27 April 2022 - 05:37

Muhtasari


•Peter alisema mkewe aligura nyumbani na kuelekea Nairobi baada ya kupigiwa simu  akiitiwa kazi.

•Mwanadada huyo alimwomba mumewe atume nauli na kumhakikishia kuwa angerudi mara moja.

Gidi na Ghost

Jamaa kwa jina Peter Amai alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Faiza ambaye walitengana naye kutokana na ugomvi wa kinyumbani.

Peter alisema mkewe aligura nyumbani na kuelekea Nairobi baada ya kupigiwa simu  akiitiwa kazi. Alifichua kuwa mkewe aliondoka bila kumfahamisha.

"Vile nilitoka kuenda kazini, niliporudi nilipata ametoka. Nilipofuatilia nilisikia ako Nairobi.  Hapo awali Alikuwa na kazi ikaisha. Alipigiwa simu akaenda," Peter alisimulia.

Peter alieleza kuwa alikuwa anamsaidia mkewe na kugharamia mahitaji yote ya nyumbani wakati kazi yake ilitamatika. Pia aliweka wazi kuwa hakuwahi kuwa na mahusiano ya  kando.

"Huwa tunaongea ananiambia nitume fare. Yeye ndiye alitoka kwa hivyo siwezi kutuma fare.  Naogopa anataka kuikula," Alisema.

Faiza alipopigiwa simu aliweka wazi kuwa sababu kuu ya kutokuwa amerejea nyumbani ni kwa kuwa Peter alikuwa amesita kumtumia nauli.

"Siwezi kukusamehea juu ata nikikuitisha pesa za nywele unakataa kutuma. Na mimi nakupenda kama sukuma. Ata nikikuitisha fare nikuje unakataa," Faiza alisema.

Mwanadada huyo alimwomba mumewe atume nauli na kumhakikishia kuwa angerudi mara moja.

"Tuma fare saa hii nikuje, ata siogi. Mimi nakupenda. Nampenda sana kama mume wangu. Yeye hanipendi sana," Alisema.

Gidi alimshauri Peter amtumie mkewe nauli ili arudi. Hata hivyo alieleza wasiwasi wake kuhusiana na utani wa Faiza.

"Nakupenda kama sukuma. Tuma fare saa hii nikuje, ata siogi!" Mwanadada amwambia mumewe


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved