logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Jamaa aachwa baada ya kuenda photoshoot na ex wake na kupakia picha WhatsApp

Alidai kuwa alikuwa amekutana na mpenzi huyo wake wa zamani kwa ajili ya kushiriki chakula  pamoja.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi23 August 2022 - 06:18

Muhtasari


  • •Ibrahim alisema marafiki wa mpenziwe walichukua screenshot ya picha iliyopakiwa kwenye WhatsApp yake na kumtumia.
  • •"Nilijaribu kumpigia ex wake simu baada ya photoshoot akaniambia kuwa wanachumbiana," Chemutai alisema
Ghost Mulee na Gidi Ogidi

Ibrahim Orata ,22, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Daisy Chemutai ,21, ambaye alimtema mapema mwaka huu.

Alieleza kuwa mpenziwe ambaye pia ni mwanafunzi mwenzake katika chuo kikuu alimuacha baada ya kipindi cha likizo.

"Vile tulienda likizo mimi nilienda kwetu naye  akaenda kwao. Nilikutana na ex wangu, mpenzi wangu alikuwa anamjua. Vile tulikutana tulipiga picha. Ex wangu alichukua simu akajipost kwa simu yangu," Ibrahim alisimulia.

Ibrahim alisema marafiki wa mpenziwe walichukua screenshot ya picha iliyopakiwa kwenye WhatsApp yake na kumtumia.

"Wakati huo mpenzi wangu hakuwa online. Marafiki wake waliscreenshot wakamtumia," Alisema.

Alidai kuwa alikuwa amekutana na mpenzi huyo wake wa zamani kwa ajili ya kushiriki chakula cha mchana pamoja.

Nilikuwa nimeongea na mpenzi wangu kuhusu mkutano wangu na ex na alikuwa amenisamehe. Lakini marafiki wake walieneza fitina na hapo akaniacha,"

Chemutai alibainisha kuwa ni ngumu sana kwake kumuamini tena Ibrahim. Alisema tayari alikuwa amemuonya dhidi ya kukutana na mpenzi huyo wake wa zamani ila akakaidi na wakaendelea kukutana.

"Ni ngumu kumsamehe kwa sasa. Siwezi kumuamini tena. Mimi nilimkataza kupatana na yeye. Walikuwa wameenda kwa photoshoot wakapiga picha na akaweka kwa status. Mimi sikuwa online," Alisema Chemutai.

Alisema aliamua kujitenga na mchumba huyo wake kwani hasira nyingi zilimpanda kila alipokumbuka yaliyojiri.

"Nilijaribu kumpigia ex wake simu baada ya photoshoot akaniambia kuwa wanachumbiana.. Yeye atie tu bidii na akipata msichana akuwe mwaminifu," Alisema.

Gidi alimshauri Ibrahim kumpatia mpenziwe muda na kutumia kipindi ambacho wametengana kujiangazia na kujirekebisha.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved