logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: “Mimi sio daktari!” Jamaa amwambia mkewe mjamzito baada ya kupata uchungu wa leba

Wakati wa kutengana kwao, Waithera alikuwa na ujauzito wa miezi saba ambao ulichangia wao kuachana.

image
na Radio Jambo

Yanayojiri27 March 2023 - 05:30

Muhtasari


•Waithera alisema ndoa yake na Kimani ilisambaratika mwezi Agosti mwaka jana kufuatia mzozo wa kinyumbani.

•Waithera alifichua kwamba alipatwa na wasiwasi baada ya Kimani kumwambia kwamba anataka kuoa mke mwingine.

Ghost na Gidi

Katika kitengo cha Patanisho, Mary Waithera (23) kutoka Nakuru alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mzazi mwenzake, Ibrahim Kimani.

Waithera alisema ndoa yake na Kimani ilisambaratika mwezi Agosti mwaka jana kufuatia mzozo wa kinyumbani. Wakati wa kutengana kwao, Waithera alikuwa na ujauzito wa miezi saba ambao ulichangia wao kuachana.

"Nilikuwa na ujauzito wa miezi saba alafu nikapatwa na uchungu wa leba. Kumwambia alisema yeye sio daktari," Waithera alisema.

Waithera alisema baadaye alijifungua mtoto wa kiume akiwa nyumbani kwao na kwa sasa mwanawe yuko na miezi mitano

"Hapo awali tulikuwa tunaongea na yeye. Lakini wiki iliyopita nilimpigia nikapata ameniblock.. Nilipata mimba nikiwa nyumbani kwetu. Alinioa nikiwa na mimba ya miezi tano. Mimba ni yake," alisema

Aliongeza, "Mama yake aliniambia niende nyumbani. Lakini yeye huwa anaenda kazi, nilijua nitapata nyumba ikiwa imefungwa,."

Mwanadada huyo alibainisha kuwa hajawahi kupokea taarifa zozote za mzazi huyo mwenzake kuoa mwanamke mwingine.

"Hata hajamuona mtoto wala kumshughulikia. Anasema ati nimpelekee mtoto akae na yeye," Waithera alisema.

Kimani alipopigiwa simu aliweka wazi kwamba hana shida yoyote na mzazi huyo mwenzake kurudi nyumbani.

"Hakuna shida, si ni kurudi tu," alisema.

Alibainisha kuwa hana tatizo lolote na mke huyo wake na kudokeza kwamba hata amewahi kumwagiza arudi.

"Mimi sijakataa arudi. Mimi sina shida na yeye.Huwa namwambia akuje alafu anaanza kuleta vituko. Huwa ananiambia ati ako mbali. Ata sijui mtoto anaitwa nani," Kimani alisema.

Ingawa hajawahi kumuona mwanawe, Kimani hata hivyo aliweka wazi kuwa mzazi huyo mwenzake hajamzuia kumuona.

Waithera alifichua kwamba alipatwa na wasiwasi baada ya Kimani kumwambia kwamba anataka kuoa mke mwingine.

Gidi alifanikiwa kuwapatanisha wawili hao na Kimani akakubali mke huyo wake arudi nyumbani.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved