Mama mkwe amfukuza mwanadada aliyeolewa na mwanawe na ujauzito wa mwanaume mwingine

Mercy alisema alikuwa amemwekeza Ezra kuhusu ujauzito wake na wakakubaliana.

Muhtasari

•Mercy alisema mahusiano yake yalisambaratika mwezi Februari baada ya mpenziwe kufunga safari ya Nairobi kwa ajili ya kazi.

•Ezra alibainisha kwamba tayari alikuwa amemweleza Mercy kuwa hataki mahusiano naye na kumtaka aache kumfuatilia.

Gidi na Ghost
Gidi na Ghost
Image: RADIO JAMBO

Kwenye kitengo cha Patanisho, Mercy Moraa (20) kutoka Nyamira alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Ezra Omosa (22).

Mercy alisema mahusiano yake yalisambaratika mwezi Februari baada ya mpenziwe kufunga safari ya Nairobi kwa ajili ya kazi.

Alisema kwamba Ezra alimchukua akiwa na ujauzito wa mwanaume mwingine na akakubali kumlea mtoto ambaye angezaliwa.

"Mimba sio yake. Wakati alinioa nilikuwa na mimba lakini sikumwambia. Ilikuwa ndoa, tumekaa miezi miwili. Alikuwa ameamua tukae naye. Kuna jamaa alikuja akamchanganyisha akamtafutia kazi ya hoteli Nairobi," alisimulia.

Mercy alisema kwamba baada ya mpenzi wake kupata kazi ya hoteli jijini Nairobi ndipo mawasiliano yao yalipotatizika.

Alisema tayari alikuwa amemwekeza Ezra kuhusu ujauzito wake na wakakubaliana. 

"Kuna siku nilimwambia niko na mimba akasema hana shida atamchukua kama mtoto wake. Watu wa kwao hawakuwa wanajua. Mamake alijua baadaye. Mamake alinifikuza kwao. Alinitupia nguo zangu nje, sijaahi kuziendea," alisema.

Alieleza kuwa ujauzito wake ni wa miezi saba.

"Ezra nampigia simu nikimueleza vile mamake alinifukuza anakata simu. Mwenye alinipachika mimba alioa. Nilienda kumpigia simu akasema niachane na yeye. Akablock namba yangu na akatafuta bibi akaoa. Nilielezea wazazi wangu. Waliniambia niachane na yeye lakini nampenda Ezra sana," alisema.

Ezra alipopigiwa simu alipigwa na butwaa kwa kuwekwa hewani.

Alibainisha kwamba tayari alikuwa amemweleza Mercy kuwa hataki mahusiano naye na kumtaka aache kumfuatilia.

"Unaniweka kwa line Radio Jambo, unafikiria nini.. Mimi nilimwambia sitaki stori zake. Mwenyewe anajua chenye alifanya," alisema kabla ya kukata simu na kutoweka.

Gidi alimshauri Mercy aache kumfuatilia Ezra na atulie nyumbani kwao hadi azae.

"Kuna mwanaume atakukubali na mtoto. Usiwe na haraka ya kuolewa na mimba," Gidi alimwambia Mercy.

Je, una ushauri upi kwa mwanadada huyo?