logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Tulikosana na mama nilipotoka kwa ndoa ya mume aliyekuwa anamtumia pesa - Brenda

" Wazazi walinitaka nizae ndio atoe mahari...” alisema.

image
na Davis Ojiambo

Vipindi18 September 2023 - 06:13

Muhtasari


  • • Mrembo huyo alisema uwa baadae jamaa huyu alimletea wale watoto wake kuishi naye lakini heshima ikawa imepotea baina yake na watoto hawa walioletwa.
GHOST NA GIDI STUDIONI

Katika kipindi cha Gidi na Ghost kwenye stesheni ya Radio Jambo asubuhi ya Jumatatu Septemba 18, mrembo kwa jina Brenda Nandaku mwenye umri wa miaka 26 kutoka mtaa wa Donholm jijini Nairobi alitaka kupatanishwa na mamake baada ya kutofautiana kuhusu yeye kwenda Saudi Arabia.

Brenda alisema kwamba mamake Elizabeth Nandaku mwenye umri wa miaka 50 alizua shida na bintiye mnamo Aprili mwaka huu baada ya Brenda kuja Nairobi kwa ajili ya mipango ya kwenda kwake Saudi Arabia.

Brenda alikuja Nairobi baada ya ndoa yake ya kwanza kugomba mwamba.

“Nilikuwa kwa ndoa ya kwanza na nikapata huko watoto 2, halafu baba ya watoto akawa hafanyi kazi nikawa mimi ndio nafanya kazi katika shule kwa kupika. Hapo kwa shule nikapata jamaa kwa shule akawa ananisaidia. Baba wa watoto alikuwa ni mhudumu wa bodaboda na hakuwa amefika nyumbani,” Brenda alisema.

Alisema kuwa huyu jamaa wa shuleni mwalimu alimpenda baadae na kumshawishi wakaoana akisema kuwa ana watoto 2 lakini mama yao alishafariki.

“Hapa shuleni nikapata huyu akawa mwalimu na nyumbani walimpenda. Aliniambia ako na watoto 2 na mke alifariki lakini kwenda kwao nilipata ako na mke na watoto 6.  Wazazi wangu walimpenda kwa sababu alikuwa anawatumia pesa kwa sababu ni walimu. Wazazi walinitaka nizae ndio atoe mahari...” alisema.

Mrembo huyo alisema uwa baadae jamaa huyu alimletea wale watoto wake kuishi naye lakini heshima ikawa imepotea baina yake na watoto hawa walioletwa.

“Tukiwa kwa nyumba akaniletea watoto wakubwa kutoka nyumbani nilijaribu kukaa nao watoto hawakujaribu kuniheshimu juu tulikuwa kama rika moja… nikasema ndio nijiondoe kwa hii ndoa nitawaambia naenda Saudia... nilipata mtoto na yeye na akachukia watoto wangu wa kwanza wawili kabisa…. Wazazi wakaniambia nisijaribu kwenda Saudi,” Brenda alieleza kwa masikitiko.

Alisema kwamba hapo ndipo mgawanyiko ulipotokea baina yake na mamake ambaye hakutaka kabisa bintiye kuodoka kwa ndoa ya yule mwalimu kwa ajili ya kwenda Saudia.

Kwa upande wake, mamake alisema kwamba asingependa kuzungumza kitu chochote kwa redio akisema kwamba bintiye anajua anapoishi na jawabu zuri ni Brenda kumfuata nyumbani azungumze naye.

"Mimi sikumfukuza mimi na yeye hatukupigana na hivyo sisemi lolote. anajua mamake anapoishi anitafute mwenyewe tuketi chini tuzungumze. Mimi ni mama yake mbona aniogope, niko mbele ya umati wa watu wengi wananisikiliza sitaki kusema mengi," mama mzazi alisema.


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved