logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Kijana ajuta baada ya kutumia 20,000 alizomwibia nyanyake kuwatumbuiza marafiki zake

Wakati huo nilikuwa mdogo, hakuna kitu ya maana nilifanya, niliwaspoil wenzangu tu." Grivin alisema.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi16 November 2023 - 06:22

Muhtasari


  • •Grivin alisema uhusiano wake na nyanyake uliharibika mwaka wa 2019 wakati alipumuibia zaidi ya shilingi elfu ishirini.
  • •Wakati huo nilikuwa mdogo, hakuna kitu ya maana nilifanya, niliwaspoil wenzangu tu." Grivin alisema.

Jamaa aliyejitambulisha kama Grivin Nyongesa Baraza ,21, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na nyanya yake Pauline Wanyonyi ,68, ambaye alikosana naye takriban miaka minne iliyopita.

Grivin alisema uhusiano wake na nyanyake uliharibika mwaka wa 2019 wakati alipumuibia zaidi ya shilingi elfu ishirini.

Alijitetea kwa kusema hajui kilichomuingia akili akafanya kitendo hicho ila akabainisha kwamba anajuta sana.

"Mwaka wa 2019, nilikuwa katika kidato cha tatu. Kuna kitu iliingia akili, sikujua ni vibaya kumuibia nyanya yangu. Niliiba zaidi ya 20,000. Alikuwa ameweka kwa kabati tu lakini nilikuwa najua funguo zake," Grivin alisimulia.

Aliongeza, "Nyanya alliita kamati ya familia tukasuluhisha lakini naona bado hayuko sawa na mimi. Wakati huo nilikuwa mdogo, hakuna kitu ya maana nilifanya, niliwaspoil wenzangu tu."

Grivin alikiri kuwa nyanya yake ndiye aliyemsomesha hadi kidato cha nne na akabainisha kuwa kitendo chake kimefanya asiishi na amani.

Alisema angependa kumuomba msamaha nyanya yake na kumuomba ampe fursa nyingine na kumpeleka katika chuo kikuu.

Bi Pauline alipopigiwa simu, Grivin alichukua fursa hiyo kumuomba msamaha,

"Kuna wakati nilikuwa nimeiba pesa zako. Nilikuwa nataka unisamehe kabisa," Grivin alimwambia nyanyake.

Bi Pauline alimwambia, "Mbona tuko na wewe kwa boma na huwezi kusema, unaenda kwa radio? Tuko na wewe kwa boma, mbona uende kutangaza kwa dunia uonekane kama mwizi. Wewe mwenyewe ndiye uliaibika ukaondoka lna mimi nilitaka usome. Nilitaka uendelee na masomo ukaambiwa uende kazi. Mimi nilikushauri usome kwanza ukakataa ukaenda. Vile ulienda hukurudi na chochote."

Kuhusu kumsamehe mjukuu huyo wake, Bi Pauline alimwambia Ghost,"Hiyo siwezi kujibu wewe. Nataka aombe msamaha tukiwa kama familia."

Grivin alikiri kujuta uovu wake na kumuomba nyanya yake amsamehe na amsaidie kurudi shule.

Je, ushauri wako kwa Grivin ni upi?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved