Steven Kimanthi ,35, kutoka Makueni alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Mirriam Nduku ,24, ambaye amekosa kuelewana naye kwa muda.
Kimanthi alisema ndoa yake ya miaka sita imekosa amani kabisa hadi kupelekea mke wake kulala kwa kiti.
“Nilioa 2018, Nimekaa na bibi yangu lakini kelele imekuwa mingi. Shida kuu huwa, mimi sina baba. Mimi ndiye nategemewa na ndugu nyumbani. Akiona nimetuma Pesa nyumbani inakuwa shida. Niko na ndugu yangu ako shule ya upili, mama yuko lakini hana uwezo,” Kimanthi alisema.
Aliendelea, “Nashughulikia familia, kila kitu kwa boma iko. Nalipa karo, chakula kwa nyumba nanunua. Shida yake hataki, anataka nikipanga pande ya wazazi wangu, pia nafanya pande ya kwao. Ata mimi niko na familia yangu nataka isonge. Juzi tumesumbuana akajitenga akaenda kulala kwa kiti. Nataka nijue kama atatoka kwa kiti ama ataendelea kulala pale.”
Mirriam alipopigiwa simu alikiri kwamba ni kweli hakuna amani nyumbani.
Alimshtumu mumewe kwa kumficha mambo mengi na kuegemea sana upande wa mama yake.
“Sikatai, lakini vile tunakaa ni kama ndugu na dada. Hatuelewani. Nikimueleza shida zangu hanisikii. Yeye hanielezi. Yeye anafanya vitu chini ya maji na hawaniambii. Yeye ni mama’s boy. Kitu huwa naona hapo ata nilikuwa nimeamua kuondoka mwaka huu. Anaweza nunua kitu afiche kwa ndugu yake. Kitu ikitendeka kwao, haniambii,” Mirriam alisema.
Kimanthi alijitetea kwa kusema, “Huwa simwambii juu nikimwambia huwa ni kelele. Ndio maana nikifanya lazima nifiche chini chini. Nikinunua kitu, akiziona inakuwa shida.”
Aliendelea kulalamika kwamba amekosa kumuelewa kabisa mkewe na akamshtumu kwa kurudi nyumbani usiku sana.
“Usitake nikuaibisha hewani. Siwezi zungusha uji na eti unanipea kila kitu.Ananiambia ataniua, saa zingine ananitoa nje usiku. Kuna siku mtoto alianguka nikamwambia, hadi wa leo hajawahi kutoa. Huyo ndiye atakununulia blender ya 15,000 ,” Mirriam alilalamika.
“Tulikosa kuelewana tangu tulipooana, sasa ni mwaka wa sita. Nakuwanga mgonjwa na hajawahi kujishughulisha, ni mara moja tu. Mimi nitajitoa,” aliongeza.
Kimanthi alimwambia, “Harakisha kujitoa, muda unaenda.. Ata nishanunua shamba lakini sijawahi kumwambia.”
Mirriam alipoulizwa kuhusu uamuzi wake wa mwisho alisema, “Yeye ndiye mwenye boma, vile ataamua ni sawa.”
Hata hivyo, alikubali ombi la mzazi huyo mwenzake la kuacha kulala kitandani.
“Nimeskia anarudi, wacha nianze kujipanga..Wewe nakupenda, lakini shida yako kuu ni kulala kwa kiti.. Hello Mirriam, I love you,” alisema Kimanthi.
Mirriam alimwambia, “Nakupenda, lakini hizo siri zako, kama tutaendelea hivyo utaona tu”Je, una ushauri gani kwa wawili hao?