Noel Mang'eno ,22, kutoka Busia alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Melisa ,22, ambaye alikosana naye hivi majuzi.
Noel alisema ndoa yake ya miaka mitano ilisambaratika wiki jana wakati mkewe alipoenda nyumbani kisha wakaanza kugombana.
"Nilikosana na mke wangu. Akienda kwao haniongeleshi. Tukiongea, ananijibu vile anataka. Akikuja huku tuko tu sawa. Huwa nashindwa ni nini mbaya. Simuelewi. Huwa namuuliza shida ni nini, haniambii. Akienda kwao hivi tu, tunakosana," Noel alisema.
Aliendelea kueleza, "Niliongea na yeye juzi. Kumuongelesha, tena tukakuja tukakosana. Niliona niache tu. Sina mtoto naye, yeye ndiye ako na mtoto. Tulichukua namba za simu ambazo zinaenda kufanana."
Kwa bahati mbaya, juhudi za kumpatanisha Noel na mkewe hazikufua dafu kwani Melisa alikuwa amezima simu yake.
Noel aliendelea kulalamika kuhusu jinsi mpenzi huyo wake huenda kanisa na kukaa siku nzima.
"Mtu akienda kanisa saa mbili asubuhi alafu anarudi saa mbili ya usiku, hiyo ni kanisa ama ni mambo mengine? Nikimpigia Jumapili kutoka asubuhi hadi jioni ananiambia ako kanisa," alisema.
Kuhusu mtoto wa mkewe, alisema, "Aliniambia alizaa akiwa kwao. Kuna mwenye alimpea mimba, kumbe alikuwa na mke na hakuwa anamwambia. Huyo mtoto wake ako ushago sijuia ana miaka mingapi. Sijawahi kumuona."
"Namuomba arudi tukae. Nitamfanyia chenye anataka. Nitamfungulia biashara," alisema Noel.
Je, una maoni au ushauri gani kwa Bw Noel?