logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mwanamke alalamika mumewe kutowajibika, kutojua kwao miaka 7 waliyoishi pamoja

Mary alisisitiza amechoka na mzazi mwenzake huku akimshtumu kwa kutowajibika katika miaka saba waliyoishi pamoja.

image
na SAMUEL MAINA

Vipindi30 July 2024 - 06:16

Muhtasari


  • •Maiyo alisema ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika Februari mwaka huu baada ya yeye kupata kazi mpya jijini Nairobi.
  • •Mary alisisitiza amechoka na mzazi mwenzake huku akimshtumu kwa kutowajibika katika miaka saba waliyoishi pamoja.

Jamaa aliyejitambulisha kama Marcel Maiyo ,34, alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Mary Lucy ,34, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Maiyo alisema ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika Februari mwaka huu baada ya yeye kupata kazi mpya jijini Nairobi.

Alisema mkewe alikosa kumuelewa wakati alipokuwa akijaribu kujipanga jijini Nairobi.

"Nilipata kazi nikakuja Nairobi. Mapato ikawa chini. Pia mapato yake ikawa chini. Alianza kushuku ni kama nimekuwa mgumu na pesa zangu. Tangu mwezi Februari aliniblock. Nilikasirika nikaanza kumtumia jumbe za matusi. Tangu Desemba nimeenda kumueleza mara kama mbili lakini alikataa kunielewa.Hakunipa nyumba nitulie. Sasa nishatulia niko sawa ," Maiyo alisema.

Mary alipopigiwa simu mara ya kwanza, aliweka wazi kwamba hana nia ya kurudiana na mzazi huyo mwenzake.

"Apana," Mary alisema.

Maiyo alijaribu kujitetea akisema, "Mimi sina ubaya na wewe. Sasa nishatulia. Naomba kama kuna mambo unaona nilikosea unieleze. Naomba unipe sheria, nifanye hii na hii ama uniunblock tuongee unieleze kile kimekuudhi kiasi hicho." 

Mary alisisitiza kwamba amechoka na mzazi mwenzake huku akimshtumu kwa kutowajibika katika miaka saba waliyoishi pamoja.

"Niongee aje kama yeye mwenyewe alishindwa kusuluhisha hiyo miaka yote. Mimi mwenye nalia kila siku. Nimechoka. Hakuwa anawajibika. Tangu aende ni nini amesaidia. Kazi yake ni kunitumia meseji za kunitishia. Nikimwambia nahitaji ananiambia niombe. Nani atakupea kila siku. Mimi nilichoka. Vile alienda Nairobi, nilipungukiwa. Nikimwambia sina, alianza kunitusi. Vile alipata kazi, nilimwambia nimefurahi hatasema nimemuacha juu hana kazi. Nilikuwa natoa kila kitu, sikuwa nalalamika," Mary alilalamika.

Maiyo alisema, "Nilikuwa nasaidia kulingana na uwezo wangu. Mimi sikuwa na kazi ya mwezi. Yeye alikuwa na kazi ya mwezi."

Mary hata hivyo aliendelea kulalamika na ata kumshtumu aaliyekuwa mumewe kwa kuwa na wanawake wengine.

"Wanawake wanakuomba pesa unawatumia. Kila mahali ni wanawake. Unaenda unalewa hata hujilewa. Mimi nimevumilia mpaka nikachoka.. Muulize hiyo miaka saba kama anajua kwetu. Mimi mwenyewe nikienda bara kila wakati nachekwa na watu. Asijaribu kuenda saai, amechelewa. Wale watoto wengine amezaa huko nje kama amewahi kuchukua akaunti zao. Niko na mtoto mwingine mmoja," Mary alisema.

Maiyo aliomba akaunti ya shule ya watoto akidai kwamba angependa kuwalipia karo, Mary hata hivyo alisikika kutoshawishika.

Je, una maoni gani ama ushauri kuhusu Patanisho ya leo?


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved