logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mume amuonya mkewe dhidi ya kuenda kazi katika nyumba za watu, atishia kutupa nguo zake nje

Rosemary alisema alianza kukosana na mume wake Agosti mwaka huu baada ya kutofautiana kuhusu suala la kazi.

image
na SAMUEL MAINAjournalist

Patanisho16 October 2024 - 08:33

Muhtasari


  • Rosemary Mukami Njeru (35) kutoka kaunti ya Embu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Peter Ng'ang'a (50) ambaye ametofautiana naye.
  • "Sitaki kukaa nyumbani, nataka kufanya kazi. Mtoto mwenye ako nyumbani ni mimi namlipia shule," alisema.

Mwanamke aliyejitambulisha kama Rosemary Mukami Njeru (35) kutoka kaunti ya Embu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Peter Ng'ang'a (50) ambaye ametofautiana naye.

Rosemary alisema alianza kukosana na mume wake Agosti mwaka huu baada ya kutofautiana kuhusu suala la kazi.

Alisema mumewe amekuwa hataki aende kazi ilhali anahitaji pesa za kumsaidia mtoto wake wa kwanza ambaye aliacha nyumbani.

"Mume wangu Hataki nikienda kushuka wateja kwao. Huwa naenda kushuka watu juu sijaweka saluni yangu. Nilijaribu kumueleza akasema wateja wakuje nyumbani badala ya mimi kuenda. Hataki nitoke," Rosemary alisema.

Aliongeza, "Kuna siku nilienda kufanya mtu blowdry, nikapata amefunga nyumba na ameenda na funguo. Alisema wakati mwingine nikienda nitapata ametupa manguo zangu nje. Tuko tu kwa nyumba lakini kazi ndio shida."

Juhudi za kumpatanisha Rosemary na mumewe kwa bahati mbaya hazikufaulu kwani Bw Ng'ang'a hakushika simu yake.

Rosemary aliendelea kusisitiza kuhusu umuhimu wa yeye kuenda kazini huku akidai kwamba yeye ndiye anasimamia mahitaji yote ya mtoto wake wa kwanza.

"Sitaki kukaa nyumbani, nataka kufanya kazi. Mtoto mwenye ako nyumbani ni mimi namlipia shule," alisema.

Je, maoni ama ushauri wako kuhusu Patanisho yako ni upi?

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved