Denis Onchuru ,27, kutoka Isinya alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Sharon Mokeira ,25, ambaye alikosana naye mwezi mmoja uliopita.
Denis alidai kwamba mkewe alimpata akiongea na mwanadada mwingine ndani ya gari yake na akawa anashuku anatoka nje ya ndoa.
"Mimi ni dereva wa teksi. Mke wangu alikuja akanipata na mrembo kwa gari. Nilimuelezea haniamini. Anasema niko na warembo wengi," Denis alisema.
Aliongeza, "Huyo nilikuwa naye alikuwa mteja. Nilimueleza hakuamini. Alinipata nikiongea na yeye kando ya barabara. Mteja aliniambia nisimamishe gari, mimi nilifikiria mteja anataka kuenda haja ndogo, nikasimamisha gari. Tulikuwa tunapiga mastori tu."
Denis hatimaye alikiri kwamba alikuwa na mahusiano ya nje.
"Enyewe ilikuwa naye lakini ilikuwa ni mahusiano kidogo tu," alisema.
Sharon alipopigiwa simu, aliweka wazi kwamba alipata jumbe za kutiliwa shaka kwenye simu ya mumewe.
"Nilipata meseji kwa simu yake, alikuwa anaongea na msichana mwingine. Ikawa inaleta shida. Ni mmoja tu nilipata," Sharon alisema.
Denis alimuomba msamaha akisema, "Nakuomba msamaha hajua nilikukosea. Turudiane tukae kama zamani. Kuja tuendelee kuzaa watoto wengi."
Sharon hata hivyo aliweka wazi kwamba hana muda wa kuzungumza na mumewe kwani alikuwa akienda mahali.
"Unaniharibia wakati," alisema kabla ya kukata simu.
Denis alisema, "Shida yake anakuwanga wa kukasirika ovyo ovyo. Alikuwa hajui password yangu, sasa nashangaa. Nilifikiria hajui password yangu, sasa nashangaa."
Gidi alimalizia kwa kumshauri Denis kuhusu jinsi ya kukaa kwenye ndoa, na kuendeleza kazi yake.
"Usikule stock na mteja tafadhali," alimwambia.
Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?