logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa aachwa baada ya msichana mwingine kushika simu yake alipopigiwa na mpenziwe, adai simu ilikuwa inacharge

"Kuna siku alipiga jioni nikakosa kushika akasema niko na mtu. Nilikuwa nimechoka sasa nilikuwa nimelala tu," Chege alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho07 November 2024 - 08:36

Muhtasari


  • Chege alisema mahusiano yake ya mwaka mmoja yalisambaratika wiki jana baada ya mchumba wake kumpigia simu ikachukuliwa na mwanadada mwingine.
  • "Mimi sina mahusiano na mwanamke mwingine. Nilikuwa nampenda sina mwingine. Anisamehe tu arudi tuanze boma," alisema.


Jamaa aliyejitambulisha kama Kelvin Chege Wanjiku ,24, kutoka Murang'a alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Mercy Cheruiyot ambaye alikosana naye hivi majuzi.

Chege alisema mahusiano yake ya mwaka mmoja yalisambaratika wiki jana baada ya mchumba wake kumpigia simu ikachukuliwa na mwanadada mwingine.

"Nilikuwa kwenye mahusiano na Mercy, tulikuwa tumepanga kuoana. Alianza kupiga piga simu nakosa kuchukua, akaanza kusema sitaki mambo yake niko na mpango wa kando. Sikuwa na mpango wa kando, ni zile tu shughuli shughuli za kazi," Chege alisimulia.

Aliongeza, "Wiki jana alipiga simu alafu ikashikwa na msichana ambaye tunafanya kazi na yeye. Simu ilikuwa kwa charge, huyo msichana akashika akamwambia siko karibu. Mimi sikuwa na mipango wa kando. Kuna siku alipiga jioni nikakosa kushika akasema niko na mtu. Nilikuwa nimechoka sasa nilikuwa nimelala tu."

Chege alisisitiza kwamba angependa kumuomba msamaha Bi Mercy na kumhakikishia kwamba hana mahusiano yoyote ya kando.

Juhudi za kumpatanisha Chege na mpenziwe hata hivyo hazikufua dafu kwani Mercy hakushika simu wakati alipopigiwa.

"Nilikuwa nimeongea na kakake akaniambia yuko huko. Alisema kwanza atulie sijui mpaka lini," Chege alisema.

Chege alimuoamba mpenziwe msamaha hewani na kumhakikishia kwamba hana mwingine.

"Mimi sina mahusiano na mwanamke mwingine. Nilikuwa nampenda sina mwingine. Anisamehe tu arudi tuanze boma," alisema.

Je, una maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved