Dorine Nekesa ,25, kutoka Bungoma alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na baba mkwe wake Chris Onyango ,50, ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.
Dorine alisema uhusiano wake na baba mkewewe uliharibika Aprili mwaka huu baada ya kuenda matanga na kukosa kurudi nyumbani.
"Niliambia baba naenda matanga akanipea pesa. Ilikuwa matanga ya ukweli. Nilikuwa na mimba na sikuwa nataka kukaa na bwanangu. Nilikuwa simpendi," Dorine alisema.
Aliongeza, 'Nilikuwa naenda naye kazi, namuona nahisi simpendi, namgombanisha na kumtusi. Alikuwa anaenda anaambia baba, alafu baba anatuita anatuongelesha."
Dorine alisema kwamba ujauzito wake kwa bahati mbaya uliweza kutoka baada ya kuenda nyumbani kwao.
"Nilienda nyumbani alafu baadaye nilienda kazi. Kazi ikawa mingi mimba ikatoka. Nilishindwa cha kuwaambia. Baba alinipigia simu nikawaambia nitarudi. Huwa namwambia tu nitarudi. Bwana yangu hakuwa anajua niko na mimba. Niliambia tu mama yangu na dada zangu," alisema.
Kuhusu kwa nini hakutaka kurudi nyumbani kwa kina bwana yake, alisema, "Niliogopa juu niliwadanganya na nikaenda nikakaa mwezi mzima. Bwana yangu alinitafuta siku za kwanza lakini siku hizi huwa hanitafuti."
"Nilikuwa nataka niombe baba msamaha kwa sababu alikuwa ananilinda kama mtoto wake. Bado niko nyumbani, kama inawezekana kurudi naweza kurudi,' aliongeza.
Bw Chris alipopigiwa simu, alimuuliza Dorine, "Umeongea na bwanako? Si yeye ndiye bwana yako, mimi ni babako tu."
Alimshauri azungumze na mume wake kabla ya kuzungumza zaidi naye.
Dorine alimwambia baba mkwewe, "Niko kwa dada yangu huku nyumbani. Sikurudi nyumbani kwa sababu nilikuwa na mimba na sikujua. Nilienda nyumbani nikagundua nilikuwa na mimba, ndiyo ilikuwa inasumbua tunagombana. Mimba ilienda ikatoka nikashindwa kuwaambia.'
Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?