Jamaa mmoja kwa jina Peter mwenye umri wa miaka 27 kutoka Kasarani ametaka kupatanishwa na mkewe ambaye waliachana mnamo mwaka 2022 baada ya kumfurusha alipompata akishiriki tendola ndoa na binamu yake.
Peter amesema kwamba alimfumania mkewe akishiriki mapenzi na binamu yake baada ya kutoka kazini na kukosa kumpata nyumbani. Kwa mujibu wa Peter, alipofika nyumbani, alimpata mkewe akiwa hayuko nyumbani na alipoenda kumwona binamu yake, alipigwa na butwaa kwa kumpata mkewe akishiriki mapenzi na binamu huyo.
Kwenye simulizi ya Peter, amesema kwamba mkewe alianza kutetemeka kutokana na uoga wa kupatikana akichepuka. Hata hivyo, Peter aliamua kuondoka sehemu hiyo na kurejea nyumabni ili kumwangalia mwanawe huku akimwacha mkewe na binamu yake nyuma. Wakati huo, Peter amesema kwamba binamu wake ambaye mama wake na mama wa Peter ni dada wa toka nitoke, alibaki akitokwa na jasho. Jaso hilo, Peter amesema lilikuwa kutokana na uoga uliomwingia binamu yake baada ya kufumaniwa.
Baada ya muda mchache wakati mkewe alirejea nyumbani, Peter alimweleza kuwa afunganye virago na kurudi kwao hadi wakati angemtaka arudi tena. Mercy aliondoka na kurejea kwao eneo la Lukhokhwe kaunti ya Bungoma huku akimwacha Peter na mwana wao mdogo.
Aidha Peter ametaka kupatanishwa na mkewe ili waendelee kuishi pamoja kama mume na mke na kulea mwanao baada ya juhudi zake za kumtafuta kutumia njia nyingine kugonga mwamba. Peter amesema kwamba alienda nyumbani kwa akina Mercy kufanya mazungumzo na familia yake.
Kwenye mazungumzo hayo, wazazi wa Mercy walimwahidi kuwa mwanao(Mercy) angalirejea baada ya muda mfupi lakini miezi mitatu baadaye, bado Mercy hajarudi kwa Peter licha ya wao kuwa na mazungumzo ya kila wakati.
Katika juhudi ya Peter kupatanishwa na Mercy, alitaka kufahamu ikiwa mkewe anapanga kurudi au la. Kwenye mazungumzo baina ya wawili hao tangu Peter kupatana na wazazi wa Mercy, mkewe amekuwa akisema kwamba angalirejea ila yuko kazini.
Peter yuko radhi kurudiana na mkewe kutokana na changamoto anazopitia katika ulezi wa mwana wao.
“Mama Gifty mimi nakupenda sana na nilitaka turidiane tuishi kama kitambo. Nakupenda sana sikutaka mtoto wangi ahangaike. Nakupenda sana tafadhali urudi tuishi.” Alisema Peter
Mercy hakupatikana kwa simu kwani nambari aliyopeana Peter iliingia
kwa mtu mwingine asiyekuwa Mercy.