logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Victor anaomba kupatanishwa na mpenzi aliyepatana naye kwenye mtandao wa facebook

Victor aliishi na Leah kuanzia Septemba 9 na kuishi kwao pamoja kulikamilika baada ya mwezi mmoja na siku chache.

image
na Brandon Asiema

Patanisho04 December 2024 - 08:59

Muhtasari


  • Victor amesema kwamba mpenzi wake aliondoka na nguo zake, malazi na kisu cha kukata mboga kati ya vifaa vingine vya nyumbani.
  • Victor alikiri kwamba alikuwa ananuia kuwatembelea wazazi wa Leah ili kuhalalisha uhusiano wao mnamo mwezi Februari mwakani. 


Victor, mwenye umri wa miaka 43, angependa kupatanishwa na mpenzi wake kwa jina Leah, 39, ambaye aliondoka nyumabni kwake takribani mwezi mmoja baada ya kuanza kuishi naye. Kwa mujibu wa Victor, alipatana na Leah kupitia mtandao wa Facebook mapema mwaka huu na kuanza mazungumzo ya kuwa na uhusiano naye.

Baada ya kuzungumza kwa muda, wawili hao waliridhia kuanzaa kuishi pamoja kama mume na mke jambo lililomfanya  Victor kumualika  Leah kwake. Leah alifika kwa Victor mwezi wa tisa tarehe na wawili hao wakaanza kuishi pamoja. Victor amesema kwamba, kwa muda waliokaa pamoja kabla ya kuondoka na vifaa vya nyumbani bila kumtaharifu Victor, Leah alikuwa anafanya shughuli za nyumbani vyema.

Victor amesema kwamba, mnamo Novemba tarehe 7 aliporudi nyumbani kutoka kazini, alipigwa na butwaa alipopata kwamba mpenzi wake ameondoka na baadhi ya vifaa vya matyumizi vya nyumbani.

“Niliporudi nyumabni kutoka kazini, sikumpata. Nilipata amebeba nguo zake, cushions za kiti, malazi, kisi cha kukata mboga, meko na shopping ya mwezi mmoja niliyokuwa nimefanya.”  Alisema Victor.

Juhudi za Gidi na Ghost kujaribu kumptanisha Victor na Leah, zilizmbulia patupu baada ya Leah kukata simu pindi tu aligundua kuwa simu aliyopokea ilikuwa ya Radio Jambo.

Aidha, Victor alikiri kwamba alikuwa ananuia kuwatembelea wazazi wa Leah ili kuhalalisha uhusiano wao mnamo mwezi Februari mwakani. Vile vile Victor amesema kwamba, tangu kuondoka kwa Leah, amekuwa akizungumza naye kwenye njia ya simu huku akimwambia kuwa angalirejea ila Victor anahisi ni kana kwamba Leah anamdanganya kwa sababu muda mrefu umepita na dalili ya kurejea kwa Leah ni finyu.

Kwenye simulizi ya Victor, mpenzi aliyempata kwenye mtandao wa Facebook, hakuwa amempa nambari za simu za wazazi wake wala watu wa karibu nae.

Awali, Victor alikuwa kwenye mahusiano na mke mwingine kabla ya kupatana na Leah ila ndoa baina yao haikudumu.



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved