Jamaa aliyejitambulisha kama Stephen Nyandiko (33) kutoka Nairobi alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mke wake Dinah Moraa (30) ambaye hajakuwa na maelewano mazuri naye.
Stephen alisema ndoa yake ya miaka minne iliingia doa kutokana na tabia yake ya kujihusisha na mipango ya kando.
Alisimulia kuhusu kisa ambapo alijihusisha kimapenzi na mke wa mtu bila kujua, jambo lililozua drama nyingi katika ndoa yake.
"Tumekuwa kwa ndoa miaka minne na tuna mtoto mmoja. Mwaka wa 2023 na 2024 nimekuwa nikihusisha na mipango wa kando. Desemba 2024 kulikuwa na mwanamke ambaye tulikuwa tunazungumza na yeye. Tulipatana na yeye, sikuwa najua kwamba ameolewa. Tuliendelea kuongea, tukapatana siku moja," Stephen alisimulia.
"Siku moja nikiwa bafu nilipata mke wangu anaongea na simu yangu. Ilikuwa mume wa yule mwanamke, huyo mwanaume akamueleza kwamba nimekuwa na mahusiano na mke wake na amevunja ndoa yake. Nilichukua simu kutoka kwa mke wangu nikamwambia sikuwa najua ameolewa. Keshoye nilipigia huyo mwanaume nikamueleza kwamba sikuwa najua ameolewa. Huyo mwanaume akasema imeisha," aliongeza.
"Bibi yangu alimuomba huyo mwanaume namba, akatumiwa screenshots za vile nimekuwa nikiongea na mke wake. Nilijaribu kuongea na mke wake lakini ikagonga mwamba. Nilicheat juu ya vile nilipata mwanamke mwenye pesa akawa ananipatia pesa kidogo kidogo,"
Dinah alipopigiwa simu, Stephen alichukua fursa hiyo kuomba msamaha.
"Naomba msamaha kwa yote nimekufanyia, naomba utafute nafasi katika moyo wako unisamehe. Sitawahi kurudia tena. Naomba turejeshe mahusiano yetu vizuri," alimwambia mkewe.
Dinah alimwambia, "Roho yangu ni ngumu kwa sababu umekuwa ukiomba msamaha, unarudia."
Pia alifunguka kuhusu jinsi mumewe amekuwa akimuonyesha upenda mwingi ilihali kwa upande mwingine anaenda nje ya ndoa.
"Nikijaribu kukumbuka yale tumepitia na wewe, tunadharauliwa na watu juu ya mahusiano yetu. Alafu unaniacha kwa nyumba. Naenda nyumbani siku mbili, kidogo ushaenda kwa wanawake mshafanya vile mmefanya. Alafu ukikuja unanionyesha upendo, yaani ata nikiambia watu ati unahanya hawawezi amini.
"Nilienda nyumbani Disemba, siku moja tu ashatafuta mwanamke amemchukua, ashaenda akalala na yeye. Yale mambo walifanya ni ya upuzi. Kibaya zaidi, mwanamke anafanya hayo mambo yote na hadelete, bwanake aliona kila kitu. Mambo yote walifanya siwezi kusema, ni ya aibu. Watu wanajua ananipenda, ananipenda ile ya uwongo. Yaani ananipenda, ata saizi naogopa kuogopa, hata watu hapa nje wakiskia watajiuliza kama ni mimi kweli. Akitoka kazini lazima apitie kwa kazi yangu. Hata juzi kuna mwanamke alikuwa anataka kujua dawa nilimpea. Watu wataona namuekelea. Huwa nachukua simu yake, naweza kaa nayo siku mzima. Amekoroga simu yake, text siwezi ona. Jioni ndiyo text zitaingia," Dinah alisema.
Stephen alisema, "Nimeamua kwamba hiyo maisha ya anasa nimeacha, narudi kwa ndoa yangu."
Dinah hata hivyo alishikilia msimamo wake kwamba kwa sasa anahitaji muda wa kufikiria.
"Roho yangu ni ngumu kwa sasa. Naskia tu niende kidogo. Ama akitaka aniache pia mimi nifanye yenye amefanya niskie vile aliskia. Kutoka wakati tulioana hajawahi kuniona na mwanaume mwingine. Anipee tu muda.. Nimejaribu kufuatilia na yule mwanamke na ni kichwa ngumu, nilijaribu kumuuliza akanitusi," alisema Dinah.
Katika maneno yake ya mwisho kwa mkewe, Stephen alimwambia, "Nimekuwa nikikuomba msamaha kwa muda, lakini nakuomba msamaha na sitawahi kurudia. Naomba unisamehe tuendelee na maisha na tuendelee kulea watoto wetu."
Dinah alimwambia, "Mi sijui chenye atafanya arudishe moyo wangu mahali ulikuwa. Kwa sasa mapenzi imeisha, siwezi kumuamini, anipee muda. Inategemea vile atakuwa."