Martin Juma mwenye umri wa miaka 32 ametaka kupatanishwa na mkewe ambaye amesema kwamba alitoka nyumbani kwake mwezi Disemba baada ya kuomba nafasi ya kwenda nyumbani kujumuika na familia wakti wa sherehe za Krisimasi.
Kwa mujibu wa Martin kumekuwepo na hali ya kutoelewana baina ya wazazi wake na wazazi wa mkewe, Martin akimshtumu mamake kumvuruga mke wake licha ya kuwa anampenda sana.
Jamaa huyo amesema kwamba mkewe kwa jina Nafula Nakhumicha mwenye umri wa miaka 29 hajarejea nyumbani tangu alipoenda licha ya yeye kutuma nauli ya kutaka mke wake arejee.
Kwa upande wa Nakhumicha, katika patanisho hiyo, alisema kwamba tayari alikuwa ameabiri piki piki ya kurejea kwa mumewe kwani Martin alikuwa amemtumia nauli lisali moja lililokuwa limepita.
Nakhumicha alisema kwamba alikuwa ameenda nyumbani kuvuna maharagwe aliyokuwa amepanda.
“Nilienda nyumbani kung’oa maharagwe yangu alafu nirudi. Ata nimechukua pikipiki narudi.” Alisema Nakhumicha.
Tatizo linguine liliibuka kwenye patanisho, Martin akisema kuwa alipigiwa simu na mama mkwe wake akimshtumu kwa kukaa na mtoto wake bila ya kulipa hata mahari, Kwa mujibu wa Martin, hakujibu madasia amabyo mama mkwe alimwambia ila aliamua kumpigia Nakhumicha kutaka kufahamu Zaidi kuhusu madai hayo.
Kwenye mawasiliano yao na mkewe, Martin alibaini kuwa mkewe alimwambia kuwa mama mkwe alikuwa na presha ndio sababu akamawambia Martin mambo hayo.
“Nilipigia mke wangu simu kumuuliza hiyo akasema mama yake alikuwa amepandisha presha.” Alisema Martin.
Kesi baina ya wachumba hawa wawili walio kwenye mahusiano na wamejaliwa na watoto wawili kwa mara nyingine ilikosa mwelekeo baada ya Nakhumicha kufichua kwamba wanaishi na Martin katika nyumba ya kukodisha ila Martin huwa hamtembelei. Licha ya Martin kukosa kumtembela huwa analipa kodi ya nyumba hiyo.
Martin aliridhia kumkombolea mkewe nyumba kutokana na matatizo yaliyokuwa yakishuhudiwa nyumbani baina ya wazazi wa Martin na mkewe.
Martin alitaka kujua msimamo wa mkewe kwani amekuwa akimtumia Nakhumicha pesa ila harejei nyumbani.
Hata hivyo, Nakhumicha alikereka na swala la Martin kumpelekakwenye patanisho akilalama kuwa anaweza kumpigia simu na wazungumze. Vi;le vile alimsuta Martin kwa kukosa akili akimtaka aboreke kwani saa moja iliyokuwa imepita, alikuwa ametuma nauli na tayari alikuwa ameabiri piki piki ya kurejea kwake.
“Yaani wewe uko na akili kweli si umenitumia transport nakuja sai. Kuwa
na akili na ukuwe mtu mkubwa.” Alimaka Nakhumicha.