logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: “Umefanya saa hii sina mke, na siwezi kuoa!” –Inauma! Jamaa Ampata Mkewe Akiwa Amemlalia Kakake Mdogo

Andrew alifichua kwamba alimfukuza mke wake baada ya tukio hilo, na hajaweza kuwaamini wanawake tena.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho07 February 2025 - 09:20

Muhtasari


  • Alex alisema nduguye alianza kumshuku kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wake, na hilo likachangia yeye kumfukuza kwake.
  • ”Ata ukiniomba msamaha, haitarejesha mke wangu. Acha tukae hivyo. Sitaki kufanyia kaka yangu kitu kibaya," Andrew alisema.

Gidi na Ghost

Kijana aliyejitambulisha kama Alex Mabuka (24) kutoka Mathare alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na ndugu yake mkubwa Andrew Malasa (27) ambaye alikosana naye mwaka mmoja uliopita.

Alex alisema uhusiano wake na kakake ulivunjika mwezi Februari mwaka jana wakati ambapo alikuwa anaishi na mkubwa huyo wake jijini Nairobi.

Alisema nduguye alianza kumshuku kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mke wake, na hilo likachangia yeye kumfukuza kwake.

“Nilikuja Nairobi kwake ili anitafutie kazi. Wakati huo nilikuwa naishi kwake. Akienda kazi asubuhi alikuwa ananiacha kwa nyumba na mke wake kwa sababu pia naye hakuwa anaenda kazi. Huo wakati ni kama yeye alinishuku, kuna siku alinipata kama tumekaa kwa kiti, akaleta shida akasema akitoka mimi nabaki tu na mke wake. Ikaleta shida hivyo mpaka akanifukuza, hakuna kitu ingine kubwa,” Alex alisimulia.

“Nilikaa kwake miezi miwili hivi. Niliwahi taka tuongee alafu akanikataza. Alisema hataki kabisa tukizungumza. Sikuwa na mahusiano na mke wake. Ni ile alikuwa anatuacha kwa nyumba, mtakosa kuongea kweli. Hamna kitu, ilikuwa kuongea tu. Mimi sikujua kitu ilifanya anifukuze,” aliongeza.

Andrew alipopigiwa simu, aliweka wazi kwamba ana uhakika mdogo wake alikuwa na uhusiano na mkewe.

Alisimulia jinsia alivyotoka kazini siku moja na kumpata mkewe akiwa amemlalia ndugu yake.

“Nina uhakika kabisa. Nilikuwa nawashuku kwa muda. Kuna wakati nilitoka kazini, kufika kwa nyumba nikapata mke wangu amelala kwa miguu zake, vile bibi na bwana hufanya. Mimi nilienda tu direct kwa bedroom, sikutaka kuzungumza zaidi ya hapo,” Andrew alisimulia.

Aliongeza, “Mke wangu vile alikuja kwa nedroom kuongea na mimi nilimwambia sitaki kufanya kitu mbaya ni afadhali aondoke. Kama mke anaweza kukufanyia hivyo na ndugu yako, anaweza kufanya nini na marafiki zako?”

Andrew alifichua kwamba alimfukuza mke wake baada ya tukio hilo, na hajaweza kuwaamini wanawake tena.

”Siwezi kurudiana naye, ata siwezi kuamini mwanamke tena,” alisema.

Alex alijaribu kumuomba msamaha nduguye akieleza kwamba makosa hayakuwa yake, lakini Andrew alisikika kushikilia msimamo wake wa kutomsamehe.

”Ata ukiniomba msamaha, haitarejesha mke wangu. Acha tukae hivyo. Sababu ya kuchukua uamuzi huu, sitaki kufanyia kaka yangu kitu kibaya. Kaa mbali na mimi. Kama hiyo ni mara ya kwanza niliwapata, mara zenye sikuwa kwa nyumb mlikuwa mnafanya nini. Mimi nakupenda kama kaka yangu ndio maana sitaki kupatana na wewe,” Andrew alimlalamikia nduguye.

Alex alisema, “Mimi nimekubali makosa. Kama unaweza kubali nikuombe msamaha, niko tayari. Wewe ni ndugu yangu. Nataka turudi tu kama kawaida.”

Andrew alimjibu, “Hilo haiwezekani, ushaniharibia maisha yangu. Kaa tu mbali na mimi kabisa. Umefanya saa hii sina mke, na siwezi kuoa. Nitakusamehea aje?”

Katika maneno yake ya mwisho kwa mkubwa wake, Alex alisema, “Mimi namuomba msamaha, na nitaendelea kumuomba msamaha mpaka ile wakati atakubali kunisamehe.”

Kwa upande wake, Andrew alimwambia, “Maisha haifanywi hivyo. Wanawake ni wengi. Azunguke huko nje atafute mke. Kama mimi ameniharibia, ameharibia wangapi huko nje. Msamaha wangu, mimi siwezi kumsamehe.”

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved