
Kijana aliyejitambulisha kama Eric Ochieng (32) kutoka
Kisumu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na Joan Akinyi (27) ambaye alikuwa
mpenzi wake.
Eric alisema mpenziwe alichukua hatua ya kumblock ghafla, bila sababu, baada ya kuchumbiana kwa takriban mwaka mmoja.
“Ata mimi sijui shida imetoka wapi. Tulikuwa tumechumbiana kwa kama mwaka mmoja. Tulishapanga tutaoana hivi karibuni. Mwezi uliopita aliamua tu kuniblock. Nikimpigia na number yoyote hashiki. Nilitaka nijue kama tunaweza kuelewana tuendelee na mahusiano,” Eric alisema.
“Mimi sikumkosea. Nashuku kuna mtu amekutana. Kuna wakati alikuja Kisumu mwaka jana Desemba na tulikaa naye siku mbili na hakuna kitu aliona kwa simu. Kurudi bado tulikuwa tunaongea. Hivi karibuni ameamua tu kuniblock. Hakuna mtu wa kwao nilijua,” aliongeza.
Joan alipopigiwa simu, aliweka wazi kwamba hana sababu haswa ya kumblock mpenziwe huyo wa mwaka mmoja.
“Hakuna kitu inaendelea. Nimemblock hivyo tu. Hakunikosea. Nilihitaji tu break. Hakuna mtu, niko serious,” alisema Joan.
Eric alimsukuma kumwambia ukweli ili ajue hatua ya kuchukua.
“Sijakublock, kama unataka kuongea na mimi nipigie moja kwa moja. Ukate simu unipigie tuongee,” Joan alimwambia.
Eric alisema, “Hana maneno mingi na ndio maana nampenda kama mke wangu.”
Joan hata hivyo alikiri kwamba mapenzi yake kwa Eric yamepungua na akasema kwamba kuna sababu.
“Kuna vile mapenzi imepungua. Kuna vitu mingi na siwezi sema, anipigie nimuelezee,” alisema.
Kwa upande wake, Eric alimwambia mpenziwe, “Bado nakupenda na vile tuliongea tukapanga ulikuwa uende nyumbani kwetu tuone. Unblock number yangu. Kama kuna mahali nilikosea naomba msamaha.”
Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?