
Mwanadada aliyejitambulisha kama Winnie Atieno (32) kutoka Kisumu alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mume wake Wilson Odhiambo (40) ambaye alikosana naye mapema mwezi huu
Winnie alisema ndoa yake ya miaka 16 ilisambaratika baada ya kutofautiana na mumewe kutokana na uraibu wake wa mchezo wa Kamari wa Aviator.
Alisema amekuwa akicheza mchezo huo kwa miaka miwili baada ya kuonyeshwa na rafikiye, na ameshindwa kabisa kuacha licha ya hasara kubwa ambayo umemletea.
“Niliingizwa kwa mchezo wa Aviator na rafiki yangu. Nimekuwa nikicheza kutoka mwaka jana. Nimecheza, inaleta hasara naendelea. Hadi mwaka huu nilisema nitaacha. Naacha alafu saa zingine napata nimecheza tena,” Winnie alisimulia.
“Juzi alikuja matanga huku nyumbani, na nilikuwa nimekaa bila kucheza. Hata simu nilikuwa nimebadilisha nikawa natumia simu ya button juu ya hiyo mchezo. Vile alikuja kwa matanga tukazika vizuri. Yeye juu alikuwa amesafiri na amechoka akalala nikachukua simu yake nikaingia kwenye account yangu nikacheza na pesa yangu ambayo nilikuwa nayo. Kwa Mpesa yake nikachukua pesa nikifikiria kwamba nitarudisha ile yangu yenye imeenda na nirudishe hiyo yake kabla aamke agundue. Kushtukia niligundua pesa yake imeenda yote, ilikuwa elfu saba na mia kadhaa. Niliamka nikamuelezea, nikamuomba msamaha. Alikasirika akavaa tu na akarudi Nairobi,” aliongeza.
Winnie alisema mumewe alikerwa sana na kitendo chake kuchukua pesa yake na kutumia yote kucheza Kamari, na amekataaa kabisa kumsamehe licha ya maombi mengi ambayo amefanya kwake.
“Nimejaribu kumuomba msamaha nimeenda hadi kwa chifu, akampigia. Aliniambia niandike barua ya kuomba msamaha na nisirudie. Niliandika akaniambie nimpee copy, niachie chifu copy na ingine nipeleke kwa polisi. Nilifanya hivyo na bado hajanisamehe. Nikimpigia, namba yangu ameweka kwa blacklist.. Hii ni wiki ya pili hatujaongea. Hachukuangi simu ata nikimpigia,” alisema.
Huku akifichua Zaidi kuhusu madhara ambayo mchezo huo umemletea, alisimulia, “Nilianza kucheza mwaka jana mwezi wa pili. Nimejaribu kuacha nikashindwa. Nimetupa hadi line nikanunua ingine, nikarudia tena, nikatupa tena, nikanunua line ingine. Nimeshikwa juu ya hii Aviator, nimelala kwa cell. Januari nilicheza nikashikwa nikalala kwa cell. Akakuja akanitoa, nikasema nitaacha. Imefika mahali nakopa pesa nacheza inaenda. Mwenyewe anakuja kunidai na ananipeleka cell. Naomba anipee nafasi ya mwisho nijaribu kuacha.’
Wilson alipopigiwa simu, Winnie alichukua fursa hiyo kumuomba msamaha na kumuahidi kwamba atarekebisha mienendo yake.
“Naomba unisamehe na sitarudia tena. Ni mara mingi umenisamehe. Naomba unisamehe mara ya mwisho na nijirekebishe. Nitajaribu nisirudie. Siwezi tafuta maisha ingine, nitapata ingine,” Winnie alimwambia mumewe.
Wilson alimwambia, “Nimekusamehe mara ngapi? Wewe nimekupatia nafasi utafute maisha ingine na mimi nitafute ingine juu kitu moja hatuwezi zungumzia miaka miwili.”
Wilson alieleza kwa undani jinsi mchezo wa Kamari umemuathiri mkewe hadi kumletea hasara kubwa.
“Huyo mama ameuza vitu zake zote amemaliza. Anacheza aviator. Pesa ya shule nawekea mtoto anachukua simu yangu anatoa anacheza nayo Aviator mtoto anarudishwa nyumbani. Mahindi namnunulia ya watoto kukula kwa nyumba anachukua anaenda anauza acheze nayo Aviator. Mwaka jana yote nimetumia zaidi ya 400k kulipa madeni. Sio Mpesa amecon watu ameshikwa nikaenda nikamtoa,” Wilson alisimulia.
Aliongeza, “Kila mara anafanya hivyo namsamehe. Tumeenda kwapolisi nimemsamehe, nimeona sina njia ingine. Nimeona nimpee nafasi atafute maisha ingine. Tumeenda kwa kanisa tukapiga magoti tukaombewa, wazee wameongea, wazazi wake wameongea. Nimechoka. Sijui amenirudisha steps ngapi nyuma. Huyo ata ameombewa. Hiyo yake sijui. Betting watu wanafanya hii yake ni ya kipekee. Ni mbaya ata nguo za mwanaume anachukua anauza. Nataka atafute maisha ingine, nimempatia nafasi.”
Wawili hao hawakuweza kupatana.
Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?
Winnie said she has taken her husband's money , has slept in cell, and has even sold things to bet.