
Elphas Momanyi mwenye umri wa miaka 25 kutoka Nyamira alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mpenzi wake Eunesta (23) ambaye alikosana naye mwezi uliopita.
Momanyi alisema uhusiano wake wa mwaka mmoja ulisambaratika mwezi Februari baada ya wao kutoka matanga ambayo ilikuwa nyumbani kwao.
Alisema mpenziwe hakupendezwa na aliyoshuhudia na kujionea nyumbani kwao, na hata akamshauri aachane na mapenzi kwanza.
“Tulikuwa tunasoma pamoja. Baada ya kujuana nikaona ako sawa akuwe dame yangu. Tukaanza kuchumbiana,’ Momanyi alisema.
“ Tumekaa mwaka moja tukiwa sawa. Mwaka jana kuna matanga ilikuwa nyumbani kwetu. Nikampigia simu nikamwambia aweze kufika. Akakaa Friday, akaenda Saturday. Ni kama hakuwa anataka tuongee lugha yetu. Baadaye alituma meseji akasema hiyo tribe yetu kuna ujinga mingi, eti tunaongea lugha yetu bila kujali kama kuna mtu. Akaniambia Zaidi kwamba hatutaendana, eti vile aliona kwetu vile kuko, I have a long way to go na niachane na mapenzi kwanza. Mimi nampenda. Hata nilikuwa nimepanga niende kwao mwezi wa tano nikutane na wazazi,” aliongeza.
Momanyi pia alieleza kutoelewa sababu ya mpenziwe kutofurahishwa na kwao “Nilimwambia aje tuongee mahali makossa iko. Akasema nimwambie tu kwa simu na akamalizia hivyo. Kisii ni Canaan, hakuna kitu inakosa Kisii. Sijui mbona anakataa Canaan.”
Eunesta alipopigiwa simu alimkana Momanyi waziwazi na kudai kwamba hawakuwahi kuwa kwenye mahusiano.
“Sasa amenipeleka kwa redio kama bibi yake ama? Sikuwa na mahusiano na yeye. Anadanganya. Ata yeye anajua hatukuwa na uhusiano. Alipoteza babake akaniambia nimpeleke matanga,” Eunesta alisema kisha akakata simu.
Momanyi hata hivyo alisisitiza kwamba alimpenda Eunesta na hata walikuwa wakipanga ndoa.
“Nilikuwa nampenda na yeye anajua hiyo kitu. Aachane na stori mingi, mimi nampenda na hiyo ni kitu alikuwa anajua tayari. Si umeskia akinikana live live. Nilikuwa nimemuonya nikamwambia ile siku tutajipata tumekosana hivi tutapatana Radio Jambo,” alisema.
Katika ujumbe wake wa mwisho kwa mpenziwe, Momanyi alisema, “Ningempenda kumwambia mimi bado nampenda sana na bado namhitaji kwa maisha yangu. Akiwa tayari akuje. Acha nijipange na yeye ajipange kidogo. Bado namhitaji.”
Je, una ushauri ama maoni gani kuhusu Patanisho ya leo?