

ONGUSH Ongura, mwanamume kutoka kaunti ya Busia ni mwanamume mwenye msongo wa Mawazo baada ya kukosana na mkewe.
Mwanamume huyo mwenye umri wa miaka 32
alipeleka mahangaiko yake kwenye kitengo cha Patanisho kwa Gidi na Ghost kwenye
Radio Jambo akiomba kupatanishwa na mkewe.
Kwa mujibu wa Ongura, walikosana na mkewe,
Naliaka Simiyu mwenye umri wa miaka 28 baada ya kuenda Saudi Arabia na kurudi
bila kurudi katika ndoa yake.
“Tumekuwa kwa ndoa kwa miaka tatu na
tuko na Mtoto moja. Nilikosana na Bibi yangu mwaka wa 2022 baada ya mimi
kukubali aende Saudi Arabia for 2yrs na alirudi May 2024. Baaya ya yeye kurudi
hata hakufika nyumbani kwangu hata kwao pia. Akisikia sauti yangu kwenye simu
anakata, mimi naomba nijue msimamo wake tu,”
Ongura alieleza.
Alieleza kwamba walitoka nyumbani kuja
Nairobi ambapo mkewe alipata nafasi ya kuenda Saudia na hadi ikaidi
wakakubaliana kutoa mimba ambayo alikuwa nayo ilia pate kusafiri.
“Nilikuwa na mke nyumbani nikakuja
Nairobi na yeye na tukaelewana akatoa mimba ili aende Saudi Arabia. Akafika huko
baada ya mwaka akanitumia pesa 40k nikajenge nyumba. Nikamwambia siwezi jenga
mpaka akuwe karibu akakasirika akaniblock. Hiyo pesa nikaongeza zingine
nikanunua pikipiki. Sasa aliporudi hakufika kwangu na kwao hajaonekana,”
Ongura alisema.
Alithibitisha kwamba mtoto ako na yeye na
mkewe hajawahi fuatilia kuhusu maendeleo ya malezo ya mtoto wao.
Gidi na Ghost walipompigia Naliaka simu,
alieleza kwamba hakuna cha kuelewana na mumewe.
Naliaka alieleza kwamba mumewe
alimuonyesha madharau baada ya kumtumia pesa kisha akazima simu, na kusisitiza
kwamba hii haikuwa mara ya kwanza bali ni mazoea ya Ongura.
“Huyo ni jamaa ambaye hasaidiki na
hakusaidii pia,” Naliaka alisema.
Hata hivyo, mwanamume huyo alikubali
makosa hayo na kusingizia ujana lakini akamuomba Naliaka kurudi kwa ajili ya
kulea mtoto na kusema kwamba kwa sasa ameshakua kiakili.
Ni ombi ambalo Naliaka alikataa katakata
kurudiana na yeye huku pia akidinda hata kutaka kumuona mwanawe.
“Nilikuachia mtoto ndio usinifuate
eti nilienda na mtoto wako. Sitaki!”
Naliaka alimwambia Ongura.
Naliaka alimaliza kwa kumfichulia Ongura ukweli kwamba kwa sasa ameshaoleka kwingine na tayari ako na mimba.