logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Jamaa na mpango wa kando wapokea kichapo cha mbwa baada ya mkewe kuwafumania kitandani

"Hiyo siku nilimpata livelive. Ata sijui nguvu ilitoka wapi, niliwatandika wote. Niliwapangusa pangusa tu kidogo," Celine alisema.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho07 April 2025 - 08:39

Muhtasari


  • "Sijui kwa nini sikufunga mlango, alitupata tukiwa bado kwa kitanda. Alinichapa mpaka wa leo naskianga mgongo bado inauma." Peter alisema.
  • Celine alipopigiwa simu alisimulia yaliyotokea na kukiri kwamba aliwapiga mumewe na mpenzi wake.

Watangazaji wa Radio Jmabo

Peter Wechenje (40) kutoka Butere alituma ujumbe akiomba kupatanisshwa na mke wake Celine Nasimiyu (32) kutoka Bungoma ambaye alikosana naye mwaka jana.

Peter alisema ndoa yake ya miaka saba ilisambaratika Februari mwaka jana wakati mkewe alitoroka baada ya kumfumania kitandani na mpango wa kando.

Alikiri kwamba mkewe alimshambulia yeye na mpenzi wake vibaya baada ya kuwapata kitandani.

"Kuna siku  mke wangu alienda kwao mwaka jana mwezi wa pili. Nilijua angekaa nyumbani siku mbili, tatu hivi. Kawaida, mambo ya wanaume kutaka kutafuta kitu ya kujiburudisha, nikajipata nimeleta mwanamke mwingine kwa nyumba. Bibi akarudi bila kuniambia na kunipata kwa nyumba na yeye," Peter alisimulia.

Aliongeza, "Alifanya vituko, akatoroka akarudi kwao, mpaka wa leo hajawahi kurudi. Alinichapa, akachapa huyo mwanamke nilikuwa na yeye. Ilikuwa sarakasi kubwa hapo kwa nyumba. Nilichapwa. Sijui kwa nini sikufunga mlango, alitupata tukiwa bado kwa kitanda. Alinichapa mpaka wa leo naskianga mgongo bado inauma. Lakini sijui nitafanya aje, nataka arudi."

Peter alikiri kwamba msichana ambaye alifumaniwa naye alikuwa ni rafiki yake wa muda mrefu, na alitumia fursa ya mkewe kutokuwepo kumualika kwake.

"Sijui ilikuwa mapepo ama. Nilijipata tu nimeita msichana tulikuwa tunajuana siku za nyuma. Vile niliona nimepata nafasi ya kuwa pekee yangu nikasema nimuite akuje, angalau tukae na yeye siku moja kabla bibi hajarudi. Kumbe bibi anarudi, sikujua. Naomba tu anisamehe, sikufanya kwa kutaka. Ni mapepo tu. Huwa nampigia tunaongea tu na watoto. Alisema hawezi rudi mpaka niende kwao. Nikaenda kwao akasema siko serious. Sasa sielewi. Ningetaka muongee na yeye arudi. Mambo ya huyo mwingine niliacha, sitaki kupigwa mara ya pili. Tangu hiyo siku ata yeye alikasirika na mimi juu ile kuchapwa alichapwa, alisema hataki tena kurudi atachapwa.," alisema.

Celine alipopigiwa simu alisimulia yaliyotokea na kukiri kwamba aliwapiga mumewe na mpenzi wake baada ya kuwapata kitandani.

"Huyo mwanaume ako na mchezo. Mimi natoka naenda nyumbani kuona wazazi. Mamangu alikuwa mgonjwa. Siku ya kurudi, nilikuwa nimemwambia ningerudi Sunday, nikarudi Saturday jioni. Mimi kurudi kwanza nakutana na viatu kwa mlango, ya pili nakutana na chupi ata sio yangu. Nikashindwa kwani kuna nini. Nikaenda jikoni nikaweka vitu nilikuwa nimetoka nazo nyumbani, tena nikatoka nje, ata hawakujua nimekuja. Nikatoka nje, nikaskia sauti ya saprano kwa bedroom yangu. Mimi kurudi nikawapata. Huyo mwanaume ako na mchezo. Lakini niliwapangusako tu kidogo," Celine alisema.

"Huyo mwanaume kila siku ni hesabu ya plus plus na hataki kupeleka watoto shule. Mpaka akuwe na akili. Kila siku tutakuwa tunakosana juu ya kitu moja? Kuna siku ingine tumekosana juu ya hiyo tu. Anapenda wanawake sana. Hiyo siku nilimpata livelive. Ata sijui nguvu ilitoka wapi, niliwatandika wote. Niliwapangusa pangusa tu kidogo," aliongeza.

Peter alichukua fursa hiyo kuomba msamaha na kuweka wazi kwamba hatawahi kurudia makosa aliyofanya.

Celine alisema bado hajarudi kwa kuwa bado aliona mumewe kama ako na mzaha. Aidha, alimtaka abadilishe tabia na line ya simu ili arudi.

"Alikuja nyumbani wakaongea. Mimi bado naona kama ako na mchezo. Juu sasa ni baba wa watoto wangu siwezi kusema hatarudi. Labda abadilishe tabia, na abadilishe hiyo line, nitarudi. Wewe mwenyewe tuma mtu alete hiyo line mimi mwenyewe nitafuta kila kitu" alisema. 

Peter alisema, "Kama bibi yangu anarudi niko tayari kufanya kila kitu anataka.. Mimi nakwambia nilikosa na sitarudia. Naomba ile mapenzi ulikuwa nayo kwangu urudishe tulee watoto wetu."

Celine alijibu, "Mimi nakupenda, najua wewe ndiye baba wa watoto wetu na hatuwezi kurudia. Nakupenda ata tukikosana."

Makala Zinazohusiana


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved