logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Patanisho: Mwanadada amwagiza mpenziwe awakusanye mipango wa kando kwenye WhatsApp Group washiriki mkutano

Alisema mpenziwe alianza kumshuku kuwa na mahusiano ya nje na ahata akapata ushahidi kwenye Facebook.

image
na Samuel Mainajournalist

Patanisho17 April 2025 - 09:15

Muhtasari


  • Ronix alisema uhusiano wake wa mwaka mmoja ulivunjika mwezi Februari wakati mpenziwe alimuacha kutokana na maneno ya mitandao.
  • Ronix alikiri alikuwa na mahusiano na wanawake wengine wawili, lakini akabainisha kwamba ameachana nao tayari.

Gidi na Ghost asubuhi

Ronix Juma kutoka Kisii alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na mchumba wake Sheila ambaye alikosana naye mapema mwaka huu.

Ronix alisema uhusiano wake wa mwaka mmoja ulivunjika mwezi Februari wakati mpenziwe alimuacha kutokana na maneno ya mitandao.

Alisema mpenziwe alianza kumshuku kuwa na mahusiano ya nje na ahata akapata ushahidi kwenye Facebook.

“Kuna vile alianza kunishuku na account yangu ya Facebook akaniomba password ya hiyo account. Nikadinda kumpea lakini kuna siku tulikutana akachukua simu yangu. Akaona kuna watu wa nyumbani tulikuwa tunachat nao na kuna dame nilikuwa nacrushia. Akakasirika akasema ananipea wakati nikimalizana na hao wasichana nimtafute,” Ronix alisimulia.

Aliongeza, “Kila wakati nikimpigia anasema kama kweli nimemalizana nao niwapigie niwaweke kwa group ya WhatsApp tuwe na mkutano.”

Ronix alikiri alikuwa na mahusiano na wanawake wengine wawili, lakini akabainisha kwamba ameachana nao tayari.

“Nilikuwa na wanawake wengine kama wawili tu. Hao wengine wawili walikuwa wa kijiji na Sheila kwao ni mbali hao walikuwa wa kuweka mtu bize tu. Ikaenda hivyo hivyo Sheila akajua ukweli akaniacha. Aliniambia nimpee wakati kidogo afikirie. Niliachana na hao wasichana niliona hakuna haja ya kukaa na watu wananiharibia,” alisema.

Sheila alipopigiwa simu alikuwa mfupi wa maneno kisha akakata simu.

“Mwambie anitafute,” alisema.

Ronix hakuwa na budi ila kukubali kumtafuta mpenzi huyo wake.

Je, una maoni ama ushauri gani kuhusu Patanisho ya leo?



RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved