
Victor Kemboi mwenye umri wa miaka 38 kutoka Eldama Ravine alituma ujumbe akiomba kupatanishwa na aliyekuwa mke wake, Sharon Chemngetich (28), ambaye alikosana naye takriban miaka mitatu iliyopita.
Victor alisema ndoa yake ya miaka saba ilivunjika mwaka wa 2022 baada ya mkewe kugundua ana mpango wa kando.
Alisema mvutano uliibuka kati ya mkewe na mpango wa kando, na akaamua kugura ndoa yake.
“Sikuwa nimeamua nioe bibi mwingine. Ilikuwa chini ya maji, alafu akanipata. Kweli nilikuwa na mpango wa kando akagundua. Mpaka kuna wakati walipigana tukafanya kesi tukamaliza. Tukaendela kukaa na yeye. Nikamfungulia hoteli,” Victor alisimulia.
Alikiri kwamba baada ya kutengana na mkewe alianza kuishi na mpango wake wa kando ambaye alimpa kazi ya upishi, ila wakaja kuachana baadaye.
“Mpango wa kando sikumuoa rasmi. Alikuwa na butchery akanipea kazi ya upishi. Nikafanya kazi yangu ya kuuza samosa hapo. Mke wangu nilikuwa nimemfungulia kazi ya hoteli. Akaanza madharau na mimi nikaanza kukaa na huyu mwingine,” alisema.
Victor alimshtumu mkewe kwa kujihusisha kimapenzi na waendesha bodaboda, ambao alikiri kuwahi kupigana nao.
“Mke wangu akaanza kuwa na vijana wengine walikuwa wanaendesha pikipiki hapo. Alikuwa anawalisha hapo kwa hoteli, nikaanza kupigana na hao vijana. Nilikuwa naskia vibaya kuona mke wangu anachukuliwa na watu wa bodaboda. Nikachoka nikaona niachane na yeye nikaenda kujitafutia. Huyo mwingine nikaachana naye pia nikaja Nairobi. Pia huyo mwingine alianza kunionyesha madharau baada ya kununua shamba naye. Saa hii ningependa mnishikanishe na huyu bibi yangu wa kwanza ndiyo hata tuweze kulea yule mtoto wetu,” alisema.
Juhudi za kumpatanisha Victor na mkewe hata hivyo ziligonga ukuta kwani Sharon alikataa kuzungumza kwa simu.
Victor alishikilia Imani kwamba mama huyo wa mtoto wake mmoja bado hajaolewa kwingine.
“Mamake angekuwa ameniambia kama ashapata mtu mwingine.Mamake aliniambia niache wasiwasi atatulia. Hakuna mtu anaweza enda kwao kwa sababu nilikuwa nimemuoa rasmi… Nashuku ako na mtu wa boda,” alisema.
Katika maneno yake ya mwisho kwa mpenziwe, Victor alisema, “Sharon
my sweetheart, my honey, bado nakupenda kwa roho yangu yote. Ata kama nimeenda,
bado nakupenda sana.”