logo

NOW ON AIR

Listen in Live

Mume wangu ni pasta mwizi, huwa wanashirikiana na wakubwa wake kuiba-Mwanamke atoboa siri

Kabla ya kuoa au kuolewa ulijua mpenzi wako kazi ambayo alikuwa anafanya kabla mpatane,

image
na Radio Jambo

Makala26 January 2021 - 21:30

Muhtasari


  • Mwanamke asema mumewe ni pasta mwizi na ambaye anashirikiana na wahubiri wa kanisa lake kuiba

Je ni siri ipi ambayo umekuwa ukijiwekea sana na kutaka kutoboa katika kipindi cha Mbusi na Lion Teketeke?

Wengi wamesaidika kupitia kutoboa siri katiika kitengo hicho.

Kabla ya kuoa au kuolewa ulijua mpenzi wako kazi ambayo alikuwa anafanya kabla mpatane, kwanini nimeuliza hili swali hii ni baada ya mwanamke mmoja kutoboa siri na kusema kwamba mumewe hajawahi mwambia kazi ambayo alikuwa anafanya hadi pale alikuwa mkewe.

 

Huku akieleza jinsi alijua mumewe ni pasta mwizi alikuwa na haya ya kusema;

"Nilipatana na mume wangu jijini Nairobi, aliponioa sikujua wala kufahamu kwamba alikuwa pasta

Baada ya muda alikuwa ananiambia anaenda kuomba kanisani, siku moja nilimfuata kisha  niajua kwamba yeye ni mdogo wa pasta

Kumbe zile siku alikuwa ananiambia anaenda maombi kanisani alikuwa anaenda kuiba vitu vya watu, kama kuku, ng'ombe na vitu vingine vingi

Sijui kama nishawahi kula pesa zake za wizi, ukienda kanisani kwao pasta yule mkubwa kwenye kanisa hilo amezingirwa na wasichana sita

Ukienda kuombewa hapo mbele, muhubiri mkubwa anakuambia ukanyage maji, ukikanyaga hao wasichana wanaanguka chini wanaanza kukutabiria

Mimi nataka kumwambia mume wangu kuwa nitamuacha kwa ajili ya tabia yake, na kutobolea washirika wa kanisa hilo siri kwamba wahubiri wao ni wezi."


RADIO JAMBO FREQUENCIES

Kisumu 100.1 | Mombasa 92.3 | Nakuru 96.9 | Eldoret 99.5 | Nyeri 99.3 | Nyahururu 97.3 | Webuye 95.3 | Meru 92.7 | Kitui 104.9 | Kibwezi 104.7 | Voi 105.7 | Malindi 98.1 | Lamu 104.7 | Narok 97.3 | Kapenguria 99.7 | Kisii 89.3 | Garissa 104.3 | Maralal 97.3 | Lodwar 92.7


logo© Radio Jambo 2024. All rights reserved