In Summary
  • Msanii Emmy Kosgei akumbuka jinsi alikejeliwa kwa ajili ya rangi ya ngozi yake

Wakenya wengi wamejitokeza na kuzungumzia na kusimulia jinsi wamekuwa wakikejeliwa hasa wasanii,waigizaji,wacheshi miongoni mwa wengine.

Kuna wale wamekuwa wakikejeliwa kwa ajili ya rangi ya ngozi yao na umbo la mwili wao.

Baadhi ya wengine upatwa na msongo wa mawazo na hata kukata tamaa maishani kwa ajili ya kejeli kutoka kwa watu na wanamitandao.

ย 

Msanii wa nyimbo za injili Emmy Kosgei kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amesimulia jinsi alijichukia kwa ajili ya kukejeliwa.

"Siwezi amini kwamba nilikuwa naogopa na nachukia rangi ya ngozi yangu ๐Ÿ™‡โ€โ™€๏ธ๐Ÿ™‡โ€โ™‚๏ธ ati eh uko mweusi sana๐Ÿ˜ƒ kama makaa.. โšซ ati ghai weee uko mweusi sana ๐Ÿ˜ƒ unakaaa.. unakaaa .. nilikuwa naingia kwa nyumba na kujiangalia ๐Ÿคฅ๐Ÿ˜ณ๐Ÿฅบ๐Ÿ™Š๐Ÿ‘€... ๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„๐Ÿ˜„ nilichukia kuitwa tuiya/cheptui," Aliandika Emmy.

Msanii huyo alisema wazazi wake walimuita cheptuiyenyuย  kwa maana walikuwa wanajivunia kuwa naye na walifahamu kuwaย  ni mrembo.

"Wazai wangu waliniita jina hilo kwa ujasiri mwingi kwa maana walikuwa wanajivunia, na kufahamu kwamba mimi ni mrembo,"

Bila ya kupinga msanii Emmy Kosgei ni mrembo na urembo wake hauna wengi.
View Comments