'Uko mweusi sana kama makaa,'Msanii Emmy Kosgei akumbuka jinsi alikejeliwa kwa ajili ya rangi ya ngozi yake

Muhtasari
  • Msanii Emmy Kosgei akumbuka jinsi alikejeliwa kwa ajili ya rangi ya ngozi yake

Wakenya wengi wamejitokeza na kuzungumzia na kusimulia jinsi wamekuwa wakikejeliwa hasa wasanii,waigizaji,wacheshi miongoni mwa wengine.

Kuna wale wamekuwa wakikejeliwa kwa ajili ya rangi ya ngozi yao na umbo la mwili wao.

Baadhi ya wengine upatwa na msongo wa mawazo na hata kukata tamaa maishani kwa ajili ya kejeli kutoka kwa watu na wanamitandao.

 

Msanii wa nyimbo za injili Emmy Kosgei kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram amesimulia jinsi alijichukia kwa ajili ya kukejeliwa.

"Siwezi amini kwamba nilikuwa naogopa na nachukia rangi ya ngozi yangu πŸ™‡β€β™€οΈπŸ™‡β€β™‚οΈ ati eh uko mweusi sanaπŸ˜ƒ kama makaa.. ⚫ ati ghai weee uko mweusi sana πŸ˜ƒ unakaaa.. unakaaa .. nilikuwa naingia kwa nyumba na kujiangalia πŸ€₯😳πŸ₯ΊπŸ™ŠπŸ‘€... πŸ˜„πŸ˜„πŸ˜„ nilichukia kuitwa tuiya/cheptui," Aliandika Emmy.

Msanii huyo alisema wazazi wake walimuita cheptuiyenyu  kwa maana walikuwa wanajivunia kuwa naye na walifahamu kuwa  ni mrembo.

"Wazai wangu waliniita jina hilo kwa ujasiri mwingi kwa maana walikuwa wanajivunia, na kufahamu kwamba mimi ni mrembo,"

Bila ya kupinga msanii Emmy Kosgei ni mrembo na urembo wake hauna wengi.