VANESSA NA ROTIMI
Vanessa Mdee na mwigizaji Rotimi waandika kitabu cha Kiswahili
Vanessa alisema kuwa amekuwa akitia bidii sana kumfunza Kiswahili mpenzi wake , Rotimi mzaliwa wa Marekani , kwani hiyo ndiyo lugha yake ya mama
•“Katika safari yangu ya kusoma Kiswahili, nataka nitembee nanyi. Mimi na mke wangu tumeandika kitabu cha Kiswahili kwa jina Swahili 101” Alisema Rotimi.
Wakizindua kitabu hicho kwenye mtandao wa Instagram, Rotimi ambaye ni mzaliwa wa Marekani kwa wazazi kutoka Nigeria amesema kuwa uandishi wa kitabu hicho ni moja kati ya hatua walizochukua ili ajue kuzungumza Kiswahili.
“Katika safari yangu ya kusoma Kiswahili, nataka nitembee nanyi. Mimi na mke wangu tumeandika kitabu cha Kiswahili kwa jina Swahili 101” Alisema Rotimi.
Vanessa alisema kuwa amekuwa akitia bidii sana kumfunza Rotimi Kiswahili kwani hiyo ndiyo lugha yake ya mama.
“Kama mnavyojua kuwa mimi nazungumza lugha tatu Kiswahili ikiwa lugha yangu ya mama, tumejifunza kutokana na uzoefu kuwa njia rahisi sana na inayofanya kazi katika kujifunza lugha ni kuitumia katika harakati zote za kila siku maishani” Mdee alisema.
Wawili hao walitaja haswa kupenda sana maneno kama ‘Asante’, ‘Nakupenda’ na ‘Mama Yangu’.
Rotimi aliagiza mashabiki wake kununua kitabu hicho kwani hio ni njia ya kusaidia bara Afrika.