(+Video) Wameweza, Hawajaweza? Bahati amshirikisha Rayvanny kwenye wimbo wa mapenzi
Bahati alitua nchini Jumatatu jioni kutoka Tanzania alikokuwa ameenda kurekodi video ya wimbo huo na Rayvanny.
•Baada ya kuachilia 'Pete Yangu' na 'Take it slow' mapema mwezi huu, Bahati sasa amewatumbuiza mashabiki wake na kibao 'Kiss' (Busu) ambacho ameshirikisha msanii matata kutoka Bongo, Rayvanny.
Mwanamuziki Kevin Bahati amezindia kibao kingine katika albamu yake 'Love like This' .
Baada ya kuachilia 'Pete Yangu' na 'Take it slow' mapema mwezi huu, Bahati sasa amewatumbuiza mashabiki wake kwa kibao 'Kiss' (Busu) ambacho ameshirikisha msanii matata kutoka Bongo, Rayvanny.
Bahati alitua nchini Jumatatu jioni kutoka Tanzania alikokuwa ameenda kurekodi video ya wimbo huo na Rayvanny.
Alikuwa ameandamana na mkewe, Diana Marua na wamekuwa Tanzania kwa kipindi cha siku tano.
Wimbo huo wa mapenzi wa Bahati na Rayvanny umepokelewa vyema na mashabiki huku ukiwa na zaidi ya watazamaji 50,000 ndani ya kipindi cha saa moja baada ya kupakiwa kwenye Youtube.
The video could not be loaded.