(+Video) Wameweza, Hawajaweza? Bahati amshirikisha Rayvanny kwenye wimbo wa mapenzi

Bahati alitua nchini Jumatatu jioni kutoka Tanzania alikokuwa ameenda kurekodi video ya wimbo huo na Rayvanny.

Muhtasari

•Baada ya kuachilia 'Pete Yangu' na 'Take it slow' mapema mwezi huu, Bahati sasa amewatumbuiza mashabiki wake na kibao 'Kiss' (Busu) ambacho ameshirikisha msanii matata kutoka Bongo, Rayvanny.

Kiss by Bahati & Rayvanny
Kiss by Bahati & Rayvanny
Image: Hisani

Mwanamuziki Kevin Bahati amezindia kibao kingine katika albamu yake 'Love like This' .

Baada ya kuachilia 'Pete Yangu' na 'Take it slow' mapema mwezi huu, Bahati sasa amewatumbuiza mashabiki wake kwa kibao 'Kiss' (Busu) ambacho ameshirikisha msanii matata kutoka Bongo, Rayvanny.

Bahati alitua nchini Jumatatu jioni kutoka Tanzania alikokuwa ameenda kurekodi video ya wimbo huo na Rayvanny.

Alikuwa  ameandamana na mkewe, Diana Marua na wamekuwa Tanzania kwa kipindi cha siku tano.

Wimbo huo wa mapenzi wa  Bahati na Rayvanny umepokelewa vyema na mashabiki huku ukiwa na zaidi ya watazamaji 50,000 ndani ya kipindi cha  saa moja baada ya kupakiwa kwenye  Youtube.

BAHATI LOVE LIKE THIS ALBUM NOW AVAILABLE ON ALL STREAMING PLATFORMS! BOOMPLAY MUSIC LINK CLICK http://Boom.lnk.to/BahatiLoveLikeThis... BAHATI & RAYVANNY SONG : KISS AUDIO: SAV BEAT VIDEO DIRECTOR: ERIS MZAVA SHOT IN DAR. TANZANIA LABEL : EMB | NEXT LEVEL | WCB #Bahati #Kiss #Rayvanny

Una hisia zipi kuhusiana na kibao hiki? Wameweza, Hawajaweza???