In Summary

•Mwanasoshalaiti Amber Ray na mke wa kwanza wa Jamal, Amira walihusika kwenye mzozano ambao ulinyima majirani usingizi na amani katika mtaa wanakoishi upande wa Syokimau mida ya saa tatu unusu usiku.

•Kwenye video ambayo Amber Ray alionyesha, wawili hao walisikika kuzozania mume wao Jamal.

Amira na Amber Ray
Image: Hisani

Drama kubwa ilishuhudiwa   maeneo ya Syokimau usiku wa Jumanne baada ya mabibi wawili wa mwanabiashara mashuhuri jijini Nairobi, Jamal Rohosafi kuhusika kwenye vita ya maneno.

Mwanasoshalaiti Amber Ray na mke wa kwanza wa Jamal, Amira walihusika kwenye mzozano ambao ulinyima majirani usingizi na amani katika mtaa wanakoishi upande wa Syokimau mida ya saa tatu unusu usiku.

Amber Ray alirekodi yote yaliyokuwa yanaendelea na kuonyesha mashabiki zaidi ya elfu kumi waliokuwa wanatazama kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Kwenye video ambayo Amber Ray alionyesha, wawili hao walisikika kuzozania mume wao Jamal.

Amber Ray alidai kuwa Amira ndiye alikuja kumshambulia kwake akiwa ameandamana na kikundi cha wanawake wengine.

"Mi niko jikoni nimefika saa hizi, waende kwanza.H ii ni nyumba yangu mimi sina shida, siingii. Ati sasa juu mimi ni bibi wa pili ninyanyaswe? Sikutongoza mwanaume wa mtu!" Amber Ray alisikika akisema.

Kwa wakati huo, wanawake ambao walikuwa wameandamana na Amira waliendelea kumzomea Amber Ray na kumtupia maneno makali ambayo hayangesikika vizuri kutokana na kelele iliyokuwa imetanda maeneo hayo.

Amber Ray ambaye pia alikuwa amejihami na marafiki wake walisikika wakiwafukuza Amira na wenzake huku wakiwaambia waende wakapeleke malalamishi yao kwa bwana yake(Jamal).

Vikundi hivyo viwili viliendelea kutupiana maneno makali na kuzomeana kwa kipindi kirefu.

Kwa wakati mmoja Amber Ray alionekana akicheza densi mbele ya kina Amira na kuwaonyesha alivyobarikiwa na nyuma nene.

(Video: Hisani; Mpasho, Amber Ray)

Amira  alimuita Amber Ray mtu anayetekeleza biashara ya kuuza mwili huku Ray akimwambia kuwa atazoea.

"Yaani leo mke mwenza amekuja kwangu kunichokora, kieleweke." Amber Ray aliskika kusema.

Kwa wakati huo muziki mkubwa ulikuwa unacheza kwenye gari moja iliyokuwa pale huku taa zake zikiwa zikimewashwa.

Mwanaume mmoja alionekana akijaribu kutuliza hali na kuwasihi Amber Ray na kikundi chake kuzima taa na muziki ila juhudi zake hazikuonekana kufua dafu.

"Hii ni nyumba yangu, anatoka kwa nini? Ako kwa nyumba yangu, ni mgeni wa hii nyumba" Amber Ray alisikika kuzuia kufurushwa kwa rafiki yake mmoja.

Maelfu ya Wakenya ikiwemo wasanii na watu mashuhuri walitazama drama hiyo yote kupitia mtandao wa Instagram.

Aliyekuwa gavana wa Nairobi, Mike Sonko alikuwa miongoni mwa waliokuwa wanatazama sinema  hiyo.

"Kwani kunaendeleaje hapa?" Sonko aliandika chini ya video iliyokuwa inaendelea.

Baadae kupitia mtandao hup wa Instagram Amber Ray alisema kuwa ndege aliyekuwa amekufa ndiye alisababisha mzozo huo.

Amber Ray akieleza kiini cha mzozo
Image: Instagram
View Comments