In Summary
  • Mapema wiki hii msanii Bahatai alitoa kibao huku akiwakashifu na kuwashambulia wasanii wenzake 
  • Vita za maneno vimezidi kushuhudiwa kwenye mitandao ya kijamii kati ya wasanii hao
butita

Mapema wiki hii msanii Bahatai alitoa kibao huku akiwakashifu na kuwashambulia wasanii wenzake huku baadhi yao wakimjibu baada ya kuona kibao chake.

Vita za maneno vimezidi kushuhudiwa kwenye mitandao ya kijamii kati ya wasanii hao.

Mchekeshaji Eddie Butita amemjibu Bahati baada ya kibao chake na kumshauri anapaswa kurudi Ukambani, kula mamebe ili awe na nguvu ya kuwakashifu wasanii wenzake.

Pia alimwambia kwamba nywele zake hazina akili kama kipara yake Bien.

"Amsheni Bahati mwambieni NimereplyFikra za Butita,"

Pia katika kibao chake Bahati aliwakashifu wasanii kama Daddy Owen,Khaligraph Jones,Ringtone, Bien miongoni mwa wengine.

Huu hapa ujumbe wake Butita kwa msanii Bahati;

"Hii ni taarifa ya hatari, yaani mtoto wa mama, unajua sauti sol walishida tuza ya mama awards,kipara ya Bien iko na akili kuliko nywele zako

Watu wamekueka sana, hata video zako zimeshindwa na msanii Samidoh sipendi udaku lakizi zile madeni ulilipa," Baadhi ya kibao chake Butita kinasema.

Hii hapa video ya mchekeshaji Butita;

 

 

 

 

View Comments