Penzi kikohozi nisamehe,'Msanii Lava Lava amuomba mpenzi wake msamaha
- Msanii Lava Lava amuomba mpenzi wake msamaha
- Mara kwa mara msanii huyo amekuwa akitoa vibao vya kuumizwa moyo, na hata vingine vya mapenzi
Msanii wa bongo Flava amabye amesajiliwa na lebo ya muziki ya WCB, Abdul Juma IddΒ marufu Lava Lava anafahamika sana kupitia kwa usanii wake.
Mara kwa mara msanii huyo amekuwa akitoa vibao vya kuumizwa moyo, na hata vingine vya mapenzi.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram aliwaacha mashabiki na gumzo baada ya kumuomba mpenzi wake Lulu Diva msamaha.
"Dah Usiku Wajana Ndosijalala Kabisa Lulu Kiukweli Achatu Ifike Mahali Mtu Aweke Wazi Penzi Kikohozi Alijifichi Nakupenda Lulu Bora Niwe Mtumwa Kwako Hakuna Jinsi inaenda Wiki Sasa Hatuelewani Naumia Binadamu Tumeumbiwa Kukosea Hakuna mkamilifu Samahani Sana Narudia Tena Samahani nisamehe Mwenzako Plz πππ₯Ίπ¦π¦π¦π¦," Aliandika Lava lava.
Kilicho washangaza mashabiki ni kuwa ni kwanini kilichowafanya wawili hao wakosane.
Hizi hapa hisia za mashabiki;
queendarleen_: Ndio na mkoo kaka @iamlavalava uko sawa wewe πππππππ
_adihuat__020: Mbn unatuletea maigizo.... ndo aina mpya ya kiki hii auππ
shebby_genius: Mapenzi mchezo pendwa wenye mashabiki wengiππππ
bonrobs_: We nae kila siku wew tyu unaumizagwaπ€£
mbe._rwa: Penzi limevuja tena ahhhhπππ