Aliyekuwa gavana wa Nairobi Mike Sonko ametoa wito kwa Wakenya kumsaidia kupatana kukutana na mganga anayedaiwa kutumia nyuki kuwashika wezi.
Kwenye mtandao wake wa Facebook Sonko alipakia video ya mzee mmoja anayeaminika kutoka eneo la Mwingi ambaye anaonekana akimeza nyoka aliye hai na kuiambatanisha na ombi la kusaidiwa kupata naye ili ampatie kazi ya kunasa mwizi.
"Naskia huyu mzee ni yule anashikanga waizi na nyuki. Hebu aletwe haraka upesi nimpe kazi. Ni watu wangapi hii kanairo mumeibiwa?" Sonko aliandika chini ya video hiyo.
Hapo awali mwanasiasa na mfanyibiashara huyo alikuwa ametangaza kwamba rafiki yake kutoka Ujerumani aliibiwa seti 25 za samani katika eneo lake la biashara mtaa wa Shanzu, Mombasa.