Malkia Karen ambaye ni mwimbaji maarufu wa Tanzania ameibua hisia kwenye mitandao tofauti ya kijamii.
Hii ni baada ya kusema kuwa hana mtoto na Diamond Platnumz jinsi watu wanavyosema.
Kulingana na majibu ambayo mwimbaji huyo alimtolea shabiki, Karen alikuwa akisema kuwa hana mtoto na Diamond na watu waache kuwahukumu vibaya.
Usemi wake Karen umeibua hisia tofauti mitandaoni, huku akifichua kwamba ataolewa akiwa na miaka 40.