Wanaume wote wanajua hawawezi kuwa waaminifu kwa mwanamke mmoja-Huddah Monroe adai
- Mwanasoshaolaiti Huddaha adai hamna mwanamume ambaye ni mwaminifu
- Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya kudai kwamba anauza tumbo la uzazi
Mwanasosholaiti Huddah Monroe amewaacha mashabiki wake na hisia tofauti baada ya kusema kwamba hawezi kuwa kwenye ndoa.
Kupitia kwenye ukurasa wake wa instagram, kwenye sekta ya hadithi za instagram HUddah alisema kwamba wanaume wanafahamu vyema kwamba hawawezi kuwa waaminifu kwa mwanamke mmoja.
Matamshi yake yanajiri saa chache baada ya kudai kwamba anauza tumbo la uzazi.
"Zaidi ya yote wanaume wanajua kwamba hawawei kuwa waaminifu kwa mwanamke mmoja,na wanadai kwamba ni biolijia ikizungumzia kuwa hivyo ndivyo wameumbwa
Wacheni kuwashinikiza wanawake,tuambieni moja kwa moja kwamba mna wengine 3 utakuwa wa nne? tukubaliane kutokubaliana," Huddah Amesema.
Huddah aliwaambiwa wanaume kwamba hana shida na wao kuwa na wanawake kumi kwani huwa inaokoa wakati wao.
"Hatuna shida nanyi mkiwa na wanawake kumi,waekeni, huwa inaokoa muda wenu , nitaamua mapema kama nitakuwa na wewe John au James sio baada ya kupata hisia
Napata kuwa una baby mama 5, watoto 25 na wake 6."