Mchekeshaji wa Churchill Show, Oliver Otieno almaarufu YY siku ya Jumanne alisema wanawake wa humu nchini hawajui kupenda.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram ,Jumanne alichapisha kanda ya video ambayo alikuwa akitoa maelezo kuhusu walivyo wanawake wa humu nchini, alieleza si lazima mwanamme ndiye mwazilishi wa mahusiano kama inavyofikirika, ila pia mwanamke anaweza kuwa na ujasiri wa kukatia mwanamme anayetamani na angetaka kuazisha mahusiano naye
"Baada ya miaka mingi ya uzoefu na utafiti wangu hatimaye nimehitimisha kuwa..... wanawake hawajui namna kutongoza wanaume. Ushawai gundua 99% ya wanawake walio jaribu kutongoza mwanamme huwa haifaulu,, unajaribu,.. unafanya kila kitu aingii. umeshindwa kabisa...alafu unafikiria umekataliwa... mmmh apana vyenye unafanya ndio shinda. "
Aliendelea kukiri wanawake huwa hawajui kuonyesha mahaba kwa wanaume, na hio usababisha mwanamme kukataa kuamini kama anapendwa kikweli.
"hamnanga saa ya mapenzi, hamnanga ata unaendelea aje? kuna huu mradi niliona ulizindua hivi majuzi unafanya vizuri. pongezi ....tumia maneno kama hizo...anzia mbali kwanza.
Isitoshe aliwaonya na hii tabia ya kuruka hatua zingine kwenye mahusiano huku akisema pia wao wakitongozwa hivo hawawezi kubali mahusiano yoyote