Hamisa Mobeto, Tanasha Donna wabarizi pamoja kudhihirisha urafikia wao
•Tanasha Donna na Hamisa Mobeto Jumapili walitumia wakati wao mwingi pamoja huku ikibanika wamekuwa marafiki wakubwa siku za hivi za karibuni.
Wapenzi wa zamani wa msanii sifika kutoka nchini Tanzania Diamond Platinumz, Tanasha Donna na Hamisa Mobetto walidhihirisha urafiki wao kwa mashabiki huku wakichapisha picha kadhaa kuonyesha ukaribu uliopo kati yao.
Siku ya Jumapili wawili hao walitumia wakati wao mwingi pamoja huku na kudhibitisha kuwa wamekuwa marafiki wakubwa siku za hivi za karibuni.
Malkia hao wawili ambao ni mama wa watoto wa Diamond wamekuwa wakidhirisha urafiki huo kwenye mitandao ya kijamii
Alhamisi wakati Hamisa Mobeto alitangaza rasmi kuwa atakuwa anazuru nchi ya Kenya,Tanasha hakuficha uchu wa kutaka msanii huyo kumtemtembelea kwake hata kama ni kwa muda tu.
Kwa mujibu wa mfululizo wa picha zinazoonekana kwenye ukurasa wao wa Instagram, wawili hao walionekana wakiwa wanabarizi pamoja katika chumba cha kifahari huku wakionekana wenye furaha kubwa.
Urafiki kati ya Tanasha na Hamisa uliimarika zaidi wakati Tanasha alimhusisha Hamisa kwenye video moja akiwa na masauti.