In Summary

•Ray C amewaeleza akina dada hasa ambao wanapenda vileo  kuwa wangalifu wanapokuwa kwenye eneo la burudani na wapenzi wao

•Hii ni kwa wale wanadada wanapenda Hennesy wewe shambulia Hennesy za watu mpaka unafika kwenye chumba hata akili ya kuchunguza camera huna hapo ndipo utajua hujui

 

Ray C
Image: istagram/Ray c

Mwanamuziki mashuhuri  kutoka Tanzania  Rehema Chalamila almaarufu  Ray C ameshauri akina dada hasa ambao wanapenda vileo  kuwa wangalifu wanapokuwa kwenye eneo la burudani na wapenzi wao.

Amesema hayo baada ya video ya uchi iliyokuwa ikienezwa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa ilikuwa ya mwanahabari mmoja wa kike wa Bongo. 

Msanii huyo amewashauri wanadada kuwa makini  wakati wanatembea  kwenye maeneo ya burudani hasa sehemu zilizowekwa  camera.

Kulingana naye.  wanadada wanapaswa kutafuta wataharamu wa kuwafunza jinsi ya kutumia simu kutambua maeneo ambayo camera zimefichwa.

"mkiwa mtandaoni jaribuni pia kujifunza mengine kupitia mtandao sio mnashinda instagram tu...kwa kifupi wanadada wenzangu hebu tafuteni wataalam wa kuwasaidia kupakua programu ambazo zinaweza kubaini sehemu zimefichwa kwnyee vyumba vya burudani mnavyoingia na waubani wenyu" alieleza Ray C

Isitishe, hakusahau kuwapa onyo wanadada wanapenda kubugia pombe hadi  kutojimbua na kufanya mambo wasiotarajia kuyafanya kwa akili zao timamu.

"Hii ni kwa wale wanadada wanapenda Hennesy wewe shambulia Hennesy za watu mpaka unafika kwenye chumba hata akili ya kuchunguza camera huna hapo ndipo utajua hujui. 

View Comments