Muthoni the Drummer Queen aeleza kwa nini amekuwa Kimya kwa muda mrefu
- Amejiunga wa wasanii maarufu ambao wanatarajia kujifungu mwaka huu.Hii ni baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu na siku ya Almahisi amejitokeza hadharani na kutangaza kuwa ana ujauzito
- amechapisha picha kudhihirisha ujauzito wake huku mashabiki wakibaki vinywa wazi kwani hawakutarajia habari za ujauzito huo
Msanii Muthoni the Drummer Queen amejiunga wa wasanii maarufu ambao wanatarajia kujifungua mwaka huu.
Hii ni baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu na siku ya Alhamisi amejitokeza hadharani na kutangaza kuwa ana ujauzito.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram amechapisha picha kudhihirisha ujauzito wake huku mashabiki wakibaki vinywa wazi kwani hawakutarajia habari za ujauzito huo.
Kulingana naye,amekuwa akipokea maswali mengi akiulizwa kwa nini ametoweka kwa mtandao na kukaa kimya huku akijibu amekuwa nyumbani.
"Nilitumia muda mwingi wa 2021 kukaa nyumbani pia kukaa mbali na wanamitandao..poleni wanamitandao, mmeona kwa nini nilikataa maombi yenu ya kibinafsi," alieleza Muthoni.
Isitoshe aliwapongeza waliokuwa wakimsaidia kuendeleza biashara zake na pia familia kwa msaada waliompa kwa takribani miezi 10 aliyokuwa kuwa nyumbani.
"Marafiki na familia wamekuwa wazuri sana katika kutushangilia na kudumisha biashara yetu, biashara yetu hadi tulipokuwa tayari kushiriki Safari hii ya miezi 10 imekuwa nzuri sana"