Muthoni the Drummer Queen aeleza kwa nini amekuwa Kimya kwa muda mrefu

Muhtasari
  • Amejiunga wa wasanii maarufu ambao wanatarajia kujifungu mwaka huu.Hii ni baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu na siku ya Almahisi amejitokeza hadharani na kutangaza kuwa ana ujauzito
  • amechapisha picha kudhihirisha ujauzito wake huku mashabiki wakibaki vinywa wazi kwani hawakutarajia habari za ujauzito huo
Muthoni the Drummerqueen
Muthoni the Drummerqueen
Image: Hisani

Msanii Muthoni the Drummer Queen  amejiunga wa wasanii maarufu ambao wanatarajia kujifungua mwaka huu.

Hii ni baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu na siku ya Alhamisi amejitokeza hadharani na kutangaza kuwa ana ujauzito.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram amechapisha picha kudhihirisha ujauzito wake huku mashabiki wakibaki vinywa wazi kwani hawakutarajia habari za ujauzito huo.

Kulingana naye,amekuwa akipokea maswali mengi  akiulizwa kwa nini ametoweka kwa mtandao na kukaa kimya huku akijibu amekuwa nyumbani.

"Nilitumia muda mwingi wa 2021 kukaa nyumbani pia kukaa mbali na wanamitandao..poleni wanamitandao, mmeona kwa nini  nilikataa maombi yenu ya kibinafsi," alieleza Muthoni.

Isitoshe aliwapongeza  waliokuwa wakimsaidia kuendeleza biashara zake na  pia familia kwa msaada waliompa kwa takribani miezi 10 aliyokuwa kuwa nyumbani.

 "Marafiki na  familia wamekuwa wazuri sana katika kutushangilia na kudumisha biashara yetu, biashara yetu hadi tulipokuwa tayari kushiriki Safari hii ya miezi 10 imekuwa nzuri sana"