'Acheni kuniita Mkunaji' Willy Paul awasihi Mashabiki

Muhtasari

•Pozee ametangaza kuwa wafuasi wake ambao wamekuwa wanamuita 'Mkunaji'  waache kumuita jina hilo mwaka huu.

•Mkunaji ni jina ambalo linahusishwa na mambo mabaya na kutokana na  jina hilo matatizo yamekuwa yakimwandana hadi wakati huu,ambapo ameamua kutangaza rasmi kuachana na jina hilo

Willy Paul
Willy Paul
Image: Instagram/willy paul

 Mwanamuziki Willy Paul almaarufu Pozee amewaomba wanamitandao ambao wamekuwa wakimuita 'Mkunaji'  wakome mwaka huu.

Pozee alieleza,  'Mkunaji' ni jina ambalo linahusishwa na mambo mabaya na kudai matatizo mengi  yamekuwa yakimkumba kutokana na jina hilo.

"Ninapenda kuchukua fursa hii kuwafahamisha wote kuwa kuanzia leo sitakuwa natumia jina la 'MKUNAJI', ni ubaya na sitaki kujihusha nalo! Tangu nilipokubali jina hilo nimekuwa na mataatizo mengi sana"alisema Pozee.

Isitoshe, alieleza wameahirisha siku ambayo walitarajiwa kutoa video ya wimbo unaojulikana 'toto' ili kusafisha jina lake kwanza huku akitaja kuwa kibao hicho kitakuwa na utofauti mkubwa kulinganisha na nyimbo zake za hapo awali.

"Tunaahirisha kuachia video ya #TOTO ili tu kuliondoa jina hili, ili tuhakikishe haliko popote. Utaona mabadiliko machache video ya #toto itakaposhuka,"

Alitaja mwaka huu wa 2022 hataki matatizo ya mwaka jana  kumfuata na hivyo kuwataka mashabiki wake wakubali  kuacha kutumia jina hilo.